Search Results
Featured, Habari, Headline »
Na Jeff Msangi
MAKALA yangu ya leo inatokana na barua pepe niliyotumiwa na msomaji wangu mmoja ambaye aliandika na kuuliza “Bro Jeff…nifanyeje ili niwe mzungumzaji mzuri mbele za watu kama vile Obama?”. Bila shaka kama tulivyo wengi wetu, msomaji huyu ni mpenzi wa Rais wa Marekani, Barack Hussein Obama.
Featured, Habari, Headline »
Na Jeff Msangi,
Bila shaka umeshawahi kusikia msemo wa wenzetu wa magharibi usemao “Time is Money”. Yawezekana kwamba msemo huo,kwa tafsiri ya moja kwa moja, unamaanisha kwamba muda ni pesa. Lakini ninavyoelewa mimi msemo huo unaongelea au unajaribu tu kuonyesha jinsi gani muda ni kitu cha thamani! Jinsi unavyoutumia muda wako hivi leo ni ishara tosha ya jinsi kesho yako itakavyokuwa.
Featured, Headline, makala »
Na Jeff Msangi
KAMA wewe sio mpenzi au msomaji wa makala zangu kila wiki, sio ajabu kwamba leo unanisoma kwa sababu umevutiwa na kichwa cha habari hapo juu! Unapenda kuongea mbele ya watu au ungependa kuwa muongeaji bora zaidi linapokuja suala la kuongea mbele za watu wengi ila umekuwa ukishikwa na uoga au mchecheto kila mara ulipojaribu kufanya hivyo.
Featured, Habari, Headline »
Jinsi ya kuamsha na kulinda ari ya kutimiza malengo yako
Na Jeff Msangi,
Kila mtu ana malengo. Tunachotofautiana ni jinsi tunavyofafanua malengo yetu na mbinu tunazozitumia ili kutimiza malengo yetu. Iwe ni kumaliza madeni uliyonayo, kuwekeza pesa kwa ajili ya kuchukua likizo ndefu,utajiri,familia bora,ndoa nzuri iliyojaa furaha,watoto wenye heshima na adabu, kufanya mazoezi ili kuwa na afya njema zaidi nk yote ni malengo ambayo binadamu hujiwekea mara kwa mara katika safari ya maisha. Wengine hufanikiwa na wengine hushindwa.

