Featured, Habari, Headline, Jamii, Siasa, makala »

[22 Mar 2014 | Comments Off | 90 views]
Katiba ikomeshe ukatili dhidi ya wanawake

MTANDAO wa Wanawake na Katiba umeainisha mambo mbalimbali ambayo ni muhimu yazingatiwe katika Katiba Mpya. Maeneo hayo yameainishwa na kutolewa ufafanuzi kama ifuatavyo;
Haki za wanawake kwenye Katiba Mpya zipewe kipaumbele stahiki:  Mtandao wa Wanawake unasisitiza haki za msingi za wanawake ziendelee kubainishwa zaidi katika Tamko la Msingi wa Haki za Binadamu (Bill of Rights), ili wanawake waendelee kupata haki sawa za uraia, siasa, uchumi  na ustawi wa jamii zinazolindwa kikatiba.
Katiba Mpya iendelee kubatilisha sheria zote za ubaguzi wa jinsia, ikiwa ni pamoja na kubagua na kudhalilisha wanawake na watoto wa …

Featured, Habari, Headline, Jamii, Uchunguzi, featured image »

[18 Mar 2014 | Comments Off | 112 views]
Ujue ugonjwa wa figo

Magonjwa ya figo
Figo hufanya kazi muhimu mwilini ambazo ni:-
• Kudhibiti na kuhifadhi virutubishi na maji na kuondoa mabaki kupitia mkojo.
• Kuchuja damu ili kuondoa mabaki ambayo ni sumu mwilini. Baadhi ya mabaki hayo ni urea, uric acid, creatinine na ammonia.
• Kudhibiti viwango vya electrolyte mwilini, yaani Sodium (Na+ ) na Potassium (K+). Sodium husaidia kudhibiti wingi wa maji mwilini na pia huwezesha mawasiliano kati ya mfumo wa fahamu na misuli (enhances commucacation between brain/nerves and muscles). Potassium husaidia mapigo ya moyo between brain/nerves and muscles). Potassimu husaidia mapigo ya moyo (regulates heart beats) …

Featured, Habari, Headline, Jamii, Siasa, Uchunguzi, featured image »

[12 Mar 2014 | Comments Off | 114 views]
JK atangaza kiama cha majangili

Rais Jakaya Kikwete amesema Serikali imenuia kumaliza kabisa ujangili nchini, ikiwa ni hatua ya kunusuru wanyama walio hatarini kutoweka katika hifadhi za taifa.
Hakusita kusisitiza kwamba, nia ya dhati ya Serikali ni kuhakikisha mkakati huo unakamilika, japokuwa kumekuwa na changamoto zinazotokana na ukubwa wa hifadhi hizo na uhaba wa vitendea kazi pamoja na askari wa wanyamapori.
Akizungumza wakati wa kupokea magari 11 ya kisasa kwa ajili ya kusaidia operesheni ya kupambana na ujangili kutoka kwa Shirika la Frankfurt Zoological Society (FZS) la Ujerumani, Kikwete alisema tatizo hilo limekuwa la muda mrefu, lakini …

Featured, Habari, Headline, Jamii, Uchunguzi, featured image »

[11 Mar 2014 | Comments Off | 146 views]
Athari za viatu vya mchuchumio  kwa wanawake

MCHUCHUMIO’ ama viatu vyenye visigino virefu, ni mojawapo ya vitu vinavyopendwa na baadhi ya wanawake mbalimbali, si katika Tanzania bali dunia nzima.
Wataalamu wanaeleza kuwa viatu hivi huharibu pingili za uti wa mgongo na huvunjavunja mifupa ya visigino.
Wanawake wenye maumbo ya kati, ambao si wanene wala wembamba wamekuwa wakipendelea viatu virefu.
Kwa kiasi kikubwa wasichana wafupi, wamekuwa wakipendelea kuvaa viatu virefu ili angalau na wao waonekane warefu.
Ashura Mgweno, mfanyakazi wa Kampuni ya Usafi jijini Dar es Salaam, anasema: “Nimetumia viatu kwa muda mrefu, lakini sasa sitaki kusikia viatu virefu. Mimi ni mfupi, …

Featured, Headline, Jamii, Uchunguzi, featured image, makala »

[9 Mar 2014 | Comments Off | 137 views]
Mlemavu asiyeona muuguzi kwa miaka 28

Pichani muuguzi Teopista Kamugisha ambaye ni mwenye ulemavu asiyeoona lakini anaifanya vema kazi yake ya uuguzi kwa miaka 28 sasa
Ni harufu ya dawa, damu,  mandhari iliyotawaliwa na bomba za sindano, dripu na mavazi meupe.
Wagonjwa wenye vidonda vya kutisha, wenye nyuso zilizojaa simanzi, wengine wanaonekana katika bonde la uvuli wa mauti na baadhi… Pengine wameshakata roho.
Hii ndiyo picha halisi ya nini maana ya uuguzi na utaipata pale tu utakapofika hospitali. Ni picha isiyopendeza machoni mwa wengi, wengi huishuhudia kwa lazima tu kwa sababu ama wanaugua au wanauguliwa. Hivyo basi Theopista Kamugisha, …