One Comment »
Maoni mapya
- Samuel on Mrisho Mpoto: Watanzania Tunakufa Kwa Roho Chafu!
- Sinzo on Waumini Wamlalamikia Askofu Jimbo La Rulenge
- Julius on Hawa Ndio Mashujaa Waliolifikisha KwanzaJamii Kwa Wanajamii Wa Njombe!
- Anonymous on Hawa Ndio Mashujaa Waliolifikisha KwanzaJamii Kwa Wanajamii Wa Njombe!
- LUDOVICK on Hawa Ndio Mashujaa Waliolifikisha KwanzaJamii Kwa Wanajamii Wa Njombe!
Zinatembelewa zaidi
- Wanaume Wana Haraka Ya Kufanya Sex - 6,040 views
- “ Tutabadilika JK Akienda Rwanda?” - 5,871 views
- Safari za JK Nje ya Nchi: - 3,768 views
- Maisha ya ujana ya Jenerali Ulimwengu, Shivji, Museveni, Sitta na wengineo UDSM - 3,666 views
- Mheshimiwa Pinda: Ya ‘ Ze Comedy’ tuwaachie kina Joti na Masanja - 3,395 views
- Wasomi wetu wanapogeuka wafagiaji mabanda ya kuku - 3,326 views
- Kalenga:Afumania Ugoni, Apofuliwa Macho - 2,363 views
- MwanaHalisi wajiandaa - 1,776 views
- JK hana dawa - 1,732 views
- KWANZA JAMII - 1,698 views
Makala mpya
- Mrisho Mpoto: Watanzania Tunakufa Kwa Roho Chafu!
- Hotuba Yangu Kwenye Uzinduzi Wa Kwanza Jamii, Njombe
- Hawa Ndio Mashujaa Waliolifikisha KwanzaJamii Kwa Wanajamii Wa Njombe!
- Kwanza Jamii Limerudi Kwa WanaJamii Njombe!
- Mrisho Mpoto Nyumbani Kwa ‘ Mwenyekiti’


Mheshimiwa Mwenyekiti
Ninayo habari ambayo imenigusa sana. Niko huku Marekani. Jana nilipigiwa simu na mdogo wangu aliyeko kijijini kwetu, milimani juu kule Umatengo, Wilaya ya Mbinga, Mkoani Ruvuma. Anasema kuwa amepewa nakala ya “Kwanza Jamii” ambayo ina makala yangu ya “Maendeleo ni Nini?” Inaonekana mhusika alinunua gazeti hili mjini Mbinga, au labda Songea.
Mdogo wangu ameniambia kuwa watu pale kijijini wamefurahi sana kusoma makala hii na wanaizungumzia sana. Ananiambia ni muhimu niendelee kuandika, maana wote wanataka hivyo.
Nimefurahi sana kuwa Mheshimiwa Mwenyekiti ulinishauri niwe naandika katika hili gazeti la “Kwanza Jamii.” Hayo ninayoyasikia kutoka kijijini kwangu yamenipa changamoto kubwa.
Halafu, mdogo wangu amekumbushia mazungumzo ambayo niliwahi kuwa na wanakijiji miaka kadhaa iliyopita, kuhusu vitabu. Nilikuwa nimetamka kuwa ningewapelekea vitabu. Sasa, kutokana na msisimko wa makala yangu katika “Kwanza Jamii,” wanakijiji wanataka nipeleke vitabu.
Ndio kusema, “Kwanza Jamii” imeleta ari ya usomaji kwa namna ya pekee pale kijijini kwangu. Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeona nikueleze hivyo, utambue ni jinsi gani “Kwanza Jamii” inavyoweza kuingia kijijini na kuchangia mabadiliko. Naahidi kuendelea kuandika makala katika “Kwanza Jamii.”
Wasalaam
Joseph L. Mbele
http://www.hapakwetu.blogspot.com