Home » Featured, makala

Safari za JK Nje ya Nchi:

2 June 2009 12,222 views 56 Comments

Profesa Joseph L. Mbele

Leo nimeamua kuongelea safari za Rais Kikwete, maarufu kama JK, katika nchi za nje. Suala hili linazungumzwa sana na waTanzania. Wako wanaodai kuwa JK anatumia muda mwingi mno nje ya nchi badala ya kubaki nchini na kushughulikia masuala ya nchi. Wako wanaodai kuwa JK anaenda kuomba omba  misaada. Wengine wanasema kazi ya kuzunguka nje ni ya waziri wa mambo ya nchi za nje, na kwamba kwa vile JK alizoea kuwa waziri wa mambo ya nchi za nje, bado hajabadilika, hata baada ya kuwa rais. Basi, kila mtu anasema yake, nami nimeona nichangie.

Naanza kwa kukiri kuwa nchi ya nje ninayoifahamu kuliko zote ni Marekani. Nimeishi na waMarekani katika nchi yao kwa miaka mingi, nikiwafundisha na kujumuika nao kwa namna mbali mbali. Naweza kusema nawafahamu, na suala la safari za JK katika nchi za nje, naweza kuliongelea kwa kutumia mfano wa Marekani.

Rais Kikwete ameshatembelea Marekani mara kadhaa, tangu awe rais. Binafsi, naona safari zake ni za manufaa. Kwanza, waMarekani kwa ujumla hawazijui nchi za Afrika kwa majina. Sana sana wanajua tu Afrika. Kuja kwa JK daima imekuwa ni fursa nzuri ya waMarekani kuijua na kuikumbuka nchi inayoitwa Tanzania. Kwa vile JK ni mtu mkubwa, ujio wake unatangazwa vilivyo, na hivi wahudhuriaji wanakuwa wengi.  Fursa ya kuitangaza Tanzania inakuwa kubwa zaidi kuliko kama angekuja mbunge au waziri kama wanavyotaka baadhi ya Watanzania. Sio rahisi mbunge au waziri aje Marekani aweze kuwavuta watu kama anavyowavuta JK.

Watanzania wanaoishi Marekani wanayo fursa ya kuitangaza Tanzania, na wako wanaofanya hivyo, kwa kadiri ya uwezo wao. Lakini mtu kama Rais Kikwete anapokuja, suala hili linakuwa na mafanikio mara dufu. Kinachosaidia zaidi ni kuwa JK ana mvuto wa pekee kwa watu. Wamarekani walishangaa kuona alivyokuwa na uhusiano wa karibu na Rais Mstaafu Bush. Na hilo niliwahi kuelezwa pia na mzee mmoja Mmarekani, ambaye ni balozi mstaafu na mtu mashuhuri. Tayari, dalili zinaonekana kuwa JK na Rais Obama wataelewana vizuri. Kwa mtazamo wangu, ziara za JK zinatuweka waTanzania kwenye chati inayohitajika vichwani mwa watu wa huku nje.

Suala la uwezo wa JK kuitangaza Tanzania nililishuhudia alipofika katika jimbo la Minnesota, Septemba 26, 2006. JK alitunukiwa shahada ya heshima ya udaktari na Chuo Kikuu cha Mtakatifu Thomas, mjini Minneapolis. Baada ya Chuo kutoa wasifu wa JK na msingi wa kumpa tuzo hiyo, JK alitoa hotuba ambamo aliwaelimisha watu wa Minnesota kuhusu hali halisi, uwezo, malengo na mahitaji ya Tanzania na Afrika. Alielezea utajiri na fursa zilizomo katika nchi yetu na bara letu. Katika kuiongelea Tanzania, alitaja rasilimali tulizo nazo, kama vile madini, ardhi ya kilimo, vivutio vya utalii, na taratibu muafaka za kuwezesha uwekezaji. Aliongelea pia hali ya kijamii na kisiasa, kuwa ni nchi ya amani,  ukifananisha na nchi zingine. Alisisitiza kuwa mazingira ya uwekezaji na ubia ni mazuri katika Tanzania na kuwa yanazidi kuboreshwa.

Hakuishia hapo, bali aliezea pia matatizo na mahitaji. Alisema kuwa pamoja na rasilimali zake, Tanzania haina uwezo wa kuziendeleza ipasavyo bila ushiriki wa wengine. Alisema kuwa Tanzania inahitaji mitaji na wawekezaji. Alisisitiza kuwa Tanzania si maskini anayehitaji kuhurumiwa na kutupiwa misaada. Inachohitaji ni washiriki katika kuufanyia kazi huu utajiri na kuleta faida kwa pande zote.

Kwa namna hii, JK alituweka Watanzania na Waafrika katika akili za WaMarekani, kwa namna tofauti na walivyozoea. Wao wamezoea kuisikia Afrika, na wengi wanadhani Afrika ni nchi ndogo, ambayo ni hoe hae kwa dhiki, njaa, maradhi na vita. JK alijenga picha tofauti miongoni mwa wali0hudhuria. Kwa yeyote anayewafahamu waMarekani, huu ni mchango mkubwa wa fikra, hasa tukizingatia kuwa vyombo vya habari viliripoti vizuri ujio wake.

Rais Kikwete alikuja na ujumbe mkubwa kutoka Tanzania, hasa wafanyabiashara. Kuja kwake na ujumbe wa wafanyabishara kulimaanisha kuwa Tanzania inataka kufanya biashara, si kuomba misaada. Ilifanyika semina kuhusu masuala ya biashara na uwekezaji Tanzania. WaTanzania wengi wanaoishi huku Minnesota walihudhuria, na walikiri  kuwa semina hii ilikuwa muhimu sana. Kwa maoni yangu, JK alitekeleza vizuri jukumu lake.

Kilichobaki ni upande wetu waTanzania. Ingekuwea bora kama  waTanzania waliohudhuria wangefanya utaratibu wa kuwaelezea wenzao ambao hawakupata fursa ya kuhudhuria, ili  kuyatafakari na kuyafanyia kazi yale ambayo yalitokana na ujio wa JK. Ulihitajika utaratibu wa sisi waTanzania kuendeleza mawasiliano na waMarekani, baada ya JK kuwahamasisha. Sisi tungepaswa tuikuze ile mbegu ambayo JK alikuwa ameipanda.

Lakini waTanzania hatukujizatiti kufanya hayo. Inawezekana wako wanaoendeleza masuala aliyoanzisha Rais Kikwete, lakini sio kama jumuia. Labda wako ambao wanafuatilia, lakini hakuna taarifa. Hatuna vikao ambapo tunaelimishana na kuhamasishana. Tunakutana tu kwenye misiba au sherehe. Kama vile ilivyo Tanzania, kwenye sherehe waTanzania tunajitokeza kwa wingi. Lakini kwenye masuala ya kushirikiana katika maendeleo, ni wazi tunahitaji kujirekebisha.

Ziara ya JK ilileta msisimko miongoni mwa watu wa Minnesota, na iliripotiwa vizuri katika vyombo vya habari. Ilikuwa ni juu yetu waTanzania kutumia fursa hii iliyotengenezwa na JK ili kuendelea kuwa karibu na watu wa Minnesota, na kuwa nao bega kwa bega, kupanga mipango na mikakati ya uwekezaji, ubia, biashara, na kadhalika.

Kwa maoni yangu, wale wanaosema JK anazunguka nchi za nje kuomba omba misaada hawasemi ukweli. Kuhusu hoja kuwa kazi ya kuzunguka nje JK awaachie wengine, sina hakika kama tutapata mafanikio kama anayoyapata yeye. Ikiwa tutamleta mbunge au waziri, sina hakika ni waMarekani wangapi watavutiwa kuja kumsikiliza. Wanaosema JK akae nchini ashughulikie matatizo ya ndani, huenda wana hoja, lakini, kwa mtazamo wangu, si rahisi kutenganisha mambo ya ndani na ya nje. Pengine kwa kujishughulisha na mambo ya nje Rais  Kikwete anajenga mazingira mazuri ya kutusaidia kwa mambo ya ndani. Vile vile Tanzania ina viongozi wengi au watu wengi ambao tunawaita viongozi. Hao wanafanya kazi gani? Kwani ni lazima awepo JK kuwaelekeza watu wa wilayani au mkoani wajibu wao? Je tunamhitaji rais aje kuwahamasisha watu wazoe taka taka mitaani, au waendeshe magari kwa uangalifu? Tunao viongozi wengi, kuanzia mtaani hadi kwenye ngazi ya Taifa. Wanafanya nini, na wanashindwa nini mpaka awepo rais?

Watanzania tumezoea kukaa vijiweni na kutoa lawama kwa wengine. Nayachukulia malamiko kuhusu safari za nje za JK kwa msingi huo. Kama kila mwananchi na kiongozi angewajibika pale alipo, nchi yetu ingekuwa mbali. Lakini hii tabia ya kumlaumu rais na kumtaka awepo nchini kutuelekeza namna ya kusafisha mitaro iliyoziba ni visingizio vya waTanzania ambao wanapenda zaidi kukaa vijiweni na kukosoa kuliko kuwajibika.

Joseph L. Mbele
1520 St. Olaf Avenue
Northfield MN 55057

Phone: 507 403 9756

http://www.josephmbele.blogspot.com

http://www.hapakwetu.blogspot.com

56 Comments »

 • kamala said:

  nimemsoooma sana huyu mzee, nashangaa ipi chema, hivi mnajua kwa nini wadada zetu wanajichubua? ni wa sababu wanataka uoneana vizuri nje ulio ndani mwao.

  sijui JK katangaza nchi wapi na wa nanina kwa ajili ya nini! labda nawaelewa wasomi sasa na ndio maana TZ inakuza uchumi mkubwa zaaidi. hivi mmareani akija ataleta nini zaidiya kulima kilimo inachoitajia kwao? ni kweli uwa tunahitaji wawekezaji wa nje wa sasa? nchi kama yetu ipi bora kati ya kuwawezesha vijana wetu kujiajiri na upata ulija au kuwakaribisha wamareani waingie ubia na watu wasiojitambua, kujiamini na wasio na cha maana cha uwauzia? hii sio kuleteleza ukoloni?

  prof anasemaje juu ya uwezekano wa ufanya kama china, yaani kujiimarisha ndani wanza badala ya nje? ipi chema, uvae upendeze jirani akutamani na kuukaribi wakati una njaa na huwezi kusimama au ule ushibe na upata afya njema harafu kwa jirani baadaye?

 • kalumekenge said:

  Prof. Mbele wape vidonge vyao hao pimbi wababaishaji ambao ni mbilikimo wa mawazo:-) Hii ya kumlaumu raisi ni visingizio wanavyotoaga wabongo yakiwashinda. Hawataki kuwajibika, kwahiyo wanatafuta wa kumlaumu badala ya kuwa wakweli. Sana sana mawaziri na ma katibu wakuu ndio wa kulaumiwa kama kazi haifanyiki kwani wao ndio watendaji na watekelezaji wakubwa, sio raisi. Kwa hili tuwe wakweli. Kwenye enzi hii na karne hii ya utandawazi kuna lazima kweli kwa raisi kuwa Tanzania ili watendaji wafanye kazi zao? Acheni visingizio vya kibongo… Mngewajibika kama raisi anavyowajibika badala ya kuendekeza vijiwe vya umbeya, nchi yetu ingekuwa mbali sana….

 • Edith Malisa said:

  Ahsante Prof. Kwa kunielimisha!

 • Martin B. said:

  Nadhani wewe Unayejiita Profesa hauko serious!! nadhani umechoka kukaa nje sasa unataka kurudi nyumbani na unataka ukifika JK akupe cheo kikubwa. Huko ni kujikombakomba sababu hujaeleza pointi yoyote ya maana!! kwani ni wangapi wameshapewa shahada za heshima za udaktari?? nyerere alipewa, mkapa alipewa. hao wote walikuwa wakisafirisafiri kama huyo unayemtetea?? Unatuambia masuala ya mvuto kwa watu!! Sisi watanzania tunataka rais mwenye kuleta maendeleo na si mvuto sababu mvuto wanao wake zetu na wachumba zetu. Mkapa hakuwa na mvuto lakini alikuwa akiheshimika sana kwa uwezo wake wa kusimamia maendeleo ya uchumi na hata akaweza kuteuliwa katika nafasi kubwa duniani kama uenyekiti wenza wa utandawazi, na pia nafasi nyingine ambayo kwa bahati mbaya nimeisahau hapa. unataka kutuambia mafanikio haya aliyapata kwa kuzurura ovyo nje ya nchi?? mimi nilitegemea wewe kama profesa utupe sababu za kitaalamu na za kichambuzi haswa kulingana na elimu yako!!!
  Halafu ninapata wasiwasi na wewe kama profesa unaposhabikia suala la rais kwenda kutafuta misaada nje!! unasema safari zake zinasaidia kupata misaada!!! naona hauko serious hapo!!! ni rais gani huyu atakaetegemea kuendesha nchi kwa kutegemea misaada??? na hivyo ndivyo alivyo JK. yeye anashindwa kuweka taratibu mzuri za kusimamia na kuzitumia rasilimali nyingi tulizonazo kuleta maendeleo, anakalia kuamini kuwa nchi itaendeshwa kwa huruma ya wahisani. ndio maana kila jambo utamsikia ”tutaongea na marafiki zetu wa nje tuone watatusaidiaje!!”. nakumbuka hata ile homa ya rift valley ilipotuvamia rais huyu alisema ”tunajaribu kuongea na wahisani tuone watatusaidiaje!!” jambo dogo kama lile!!. Hayo ndio mambo ambayo wewe kama profesa unayaona yanafaa? ina maana siku ukipata nafasi ya kuongoza hii nchi utategemea kuiongoza kwa misaada hata wewe??
  Gazeti la the economist lilipata kuchambua kwa kina kuhusu safari hizi za JK na walifanya analysis ya kiuchumi na iliyokwenda shule haswa. acha hii iliyonukuliwa na gazeti la mwananchi hapa juzi hii haikusema chochote. Ninayoiongelea mimi ilitoka mwaka 2007 mwanzoni!
  Halafu unaongelea suala la rais kuwa na uhusiano wa karibu na Bush so what professor?? Uhusiano huo unatusaidia nini watanzania maskini iwapo hata hiyo misaada hatuoni madhara chanya yake?? na je kwani kuomba misaada ni lazima usafiri?? kwa nini safari zake haziishi na kila aendapo huandamana na jopo kubwa la watu kitu ambacho ni kuchoma bure pesa ya mlipa kodi??. Mimi nasema huku kusafiri mara kwa mara ni ishara ya rais wetu kukosa mbinu zinazotakiwa katika kuendesha nchi namaanisha katika kuleta maendeleo na badala yake wewe na yeye mnadhani nchi huendeshwa kwa misaada huku tukiachia rasilimali zikifujwa bila manufaa kwa wananchi!! wewe leo kama profesa unaongea hivyo, balozi wa afrika kusini yeye alisema kwamba Kwa rasilimali zilizopo Tanzania basi Tanzania ilitakiwa kuwa ni nchi inayotoa misaada kwa nchi nyingine!!! unaona jinsi mnavyotofautiana mawazo?? mimi nathubutu kusema kabisa profesa umeandika makala bila kutoa sababu za kitaalamu zinazoweza kutufanya tuione kama makala yenye kiwango cha kuandikwa na profesa na badala yake umejaza ushabiki tu ndani ya makala yako na hii inanitia shaka kidogo. Nadhani kama profesa unatambua kuwa kama nchi tunatakiwa kujitegemea! Tunapojitegemea tunapunguza presha kutoka nje. Tunapunguza uwezekano wa mataifa ya nje kutuamrisha na hata kutuamlia jinsi ya kusimamia rasilimali zetu. Na njia pekee ya kujitegemea ni kupunguza utegemezi wetu kwa mataifa ya nje. Kupunguza utegemezi wa bajeti yetu kwa wahisani. Kwa maana nyingine kupunguza misaada au kuombaomba!! Sasa wewe unashabikia kuombaomba profesa!! Kenya sasa hivi wanaendesha bajeti yao kwa karibia 85% na malengo yao ni kuona kuwa wana-finance bajeti yao kwa 100%, wakati sisi bado 40%-45% ya bajeti inategemea wahisani!! Ukumbuke kuwa rais Kibaki hana safari zisizo na maana kama hizo unazozishabikia wewe profesa. Ukumbuke kuwa Kenya hawana rasilimali zinazoweza kulingana na hizi zilizopo Tanzania. Almas nyingi, Dhahabu nyingi sana sana, Tanzanite duniani kote inapatikana tanzania tu, Mafuta, Rubi, Makaa ya mawe, maziwa nk vyote hivi ni vitu ambavyo kama vingesimamiwa vizuri nchi ingeweza kabisa kujitegemea kuliko kukalia misaada. Leo hii tunapewa misaada na Uholanzi nchi ambayo mbali na bahari tena dogo haina chochote!!Misaada hiyo tumeanza kupewa leo?? si tangu enzi misaada tunapata mbona hatuoni impact yake ofcourse impact ipo lakini si ya kiwango kinacholingana na thamani ya misaada yenyewe!!
  Ukweli ni kwamba rais wetu anapenda safari ambazo zimekuwa nyingi sana na zisizo na manufaa yoyote kiuchumi zaidi ya kuongeza tu gharama ya uendeshaji nchi!!
  Bwana Joseph Mbele mimi binafsi nitatofautiana na wewe milele katika pointi zako ulizoziandika. Hazina uchambuzi yakinifu. Ningekuomba tu uache kutetea mambo ambayo yako wazi kabisa na kwa kuonyesha wazi kabisa kuwa una personal interests.
  Ahsante
  Martin Bugoye
  GA, USA.

 • Ludigo said:

  Asante sana kwa kuelimisha jamii kuhusu safari za Rais.Mimi nitakuwa tofauti na wewe kidogo sana,si ninakupiga hapana.Nachangia nini kifanyike ili nchi yetu iendelee vizuri.Wawekezaji tunawaitaji ili kuboresha uchumi wetu wanatakiwa wafanyiwe environmental evaluation.Ili rasimali zetu zisiishe na wao kupmbia na kutuachia jangwa lisilo na kitu hata kimoja.Tukionglelea wakezaji kwa mfano sekta ya utalii,kinachoendelea hapa ni depletion of resources na sio kuimalisha viboresha uchumi wetu.kitendo cha serikali kutoa leseni za kuwinda wanyama pori[professional huntering].Na kuua wanyama ambao hata hakuna utafiti wowote ule unaoonyesha wapo wengi kama wanavyofikiria watu wengi.Hii ni hatari kwa uchumi wa nchi yetu.tuna mfano hai hapa,Nchi yetu ilikuwa ni moja kati ya nchi chache zenye Faru kwa wingi.Seikali kutojua au kutotazama mbele walisaidia kupotea kwa hao faru kwa kasi ya ajabu.WE ARE HEADING TOWARD ECOLOGICAL BANKRUPTCY SOON.Vile vile serikali inasaidia wawekezaji kujenga hotels ndani ya mbuga.Kitendo hicho kinawafanya wanyama wa pori wawe hatarini kukamatwa kiurahisi na maadui zao[predator].Hotel zinatakiwa zijengwe sehemu moja si zijengwe kama uyoga ndani ya mbuga.Na watanzania tujue kuwa Mungu ametujalia kweli kweli sisi watanzania.Tunaitaji watu smart kuweza kumshauri Rais na Kila mtu saidie kutunza rasilimali zetu.Njia pekee ya kuufanya uchumi wetu kuwa sustainable ni kuboresha hiyo rasimali zaidi kuliko ulivyoikuta.kila mwaka kwa mfano mbuga inakuwa more natural.sasa hao wawekezaji wanakuja hakuna mtu ambae ana ujari ecological demage.HOTELI ZINATAKIWA ZIWE GREEN-HOTELS.NA ZIFANNANE NA MAZINGIRA YA PORI.NA ZILE MOBILE ,YAANI YANAWEZAKANA KUHAMA PALE ONCE TUMEONA KUNA HADHARI KWA WILDERNESS.TANZANIA INACHOFANYA SASA KUWAITA WAWEKEZAJI KUWEKEJA BILA KUJARI HADHARI ZA MUWEKEZAJI NAWEZA KUITA NI “CONSUMPTION ECONOMY”.AND SHORT TERM PROFIT INVESTMENT.
  MUNGU IBARIKI TANZANIA.
  MDAU [ENVIROMENTALIST]
  WASHINGTON DC

 • Anonymous said:

  Great comment!

 • bwana mawazo said:

  maelezo ya ndugu Mbele kuunga mkono ziara za ndugu Kikwete nchi za nje mara kwa mara ni haki yake, lakini ukweli unabaki pale kwamba ziara hizo hazina faida kwa nchi yetu. Hii ni aibu kubwa kuwa na kiongozi anaezurura duniani kuomba omba misaada.msimamo wa azimio la arusha unasema hivi kuhusu kuomba omba fedha:
  “Hii ndiyo imani yetu ya sasa. Viongozi wa TANU mawazo yao ni kwenye ongozi wa Serikali, wanasiasa na watumishi,mawazo yao na matumaini yao ni kwenye fedha. Viongozi wa wananchi na wananchi wenyewe katika TANU, NUTA, Bunge, UWT.,Vyama vya Ushirika, TAPA na makundi mengine ya wananchi,mawazo yao na maombi yao na matumaini yao ni FEDHA. Ni kama ote tumekubaliana na tunasema kwa sauti moja, “Tukipata fedha
  tutaendelea, bila fedha hatutaendea”!
  sababu kubwa ya ziara hizi ni kuomba hawa wakubwa watusaidie kuendeleza nchi yetu. azimio la arusha linasema tena:
  “Ni jambo la kijinga kuchagua fedha kuwa ndiyo chombo chetu
  kikubwa cha maendeleo na hali tunajua kuwa nchi yetu ni maskini.
  Ni ujinga vile vile, kwa kweli ni ujinga zaidi, tukidhani kuwa tunaweza kuondoa hali hii ya unyonge wetu kwa kutegemea fedha za kutoka nje badala ya fedha zetu wenyewe.”
  Kwa kipimo hiki cha Azimio la Arusha hivi sasa Tanzania ina kiongozi mjinga anaetegemea wakubwa toka nje kuiletea Tanzania neema ndio maana hizi safari zisizokwisha.
  mimi sijui kama Ndugu Mbele amewahi kusoma azimio la arusha, au sasa na yeye amelitosa baharini kama Ndugu Kikwete, kwani azimio linasema hivi kuhusu wawekezaji na misaada toka amerika na ulaya:
  “Kama tungeweza kushawishi wenye raslimai wa kutosha kutoka
  Amerika, na Ulaya kuja kwetu na kuanzisha Viwanda vyote, na
  mipango mingine yote ya uchumi tunayohitaji katika nchi hii, hivi
  kweli tungekubali bila kujiuliza maswali? Tungekubali kweli kuacha
  uchumi wetu wote uwe mikononi mwa wageni kwa ajili ya kupata
  faida na kuipeleka katika nchi zao? Hata kama wasingedai
  kuhamisha faida na kupeleka makwao, bali faida yote watakayopata
  wataitumia hapa hapa Tanzania kwa maendeleo zaidi. Hivi kweli
  tungekubali jambo hili bila kujiuliza hasara zake kwa Taifa letu?”
  hatuwezi kujenga taifa kwa kutegemea wageni.
  kuhusu ziara hizi za Ndugu yangu Jakaya Kikwete, azimio lilikwisha eleza wazi:
  “Juhudi yetu ya kutafuta fedha inazidi kuongezeka! Sio kwamba
  tuipunguze, bali, badala ya safari nyingi ndefu na zenye gharama
  kubwa za kwenda kutafuta fedha za maendeleo yetu, itafaa kufunga
  safari kwenda vijijini kuwafahamisha na kuwaongoza wananchi katika
  kujiletea maendeleo kwa juhudi yao wenyewe. Ndiyo njia ya kweli ya
  kuleta maendeleo kwa kila mtu.”
  anaepinga haya haitakii mema Tanzania! Mungu ibariki Tanzania na watu wake utupe viongozi wenye hekima!

 • mayor said:

  Nashukuru,prof mbele kwa maoni yako.
  ukweli watanzania ni watu ambao mara nyingi huwa tunapenda kulaumu vitu mbavyo hata havistahili kulaumiwa.nimepata changamoto yako prof kwa muono tofauti na watanzania walio wengi,na ninadhani hii inatokana na kuishi nje ya nchi kwa muda mrefu hivyo umeona tofauti ya mtazamo wa utendaji wa serikali(hususan mheshimiwa raisi jk )WATANZANIA WIMBO MBAYA HAULEI MTOTO.TUSIKALIE TUU,UFISADI,SAFARI ZA VIONGOZI,NA MENGINE MENGI.ambayo huwa tuna laumu serikali na viongozi siku zote.serikali sio mtu mmoja hata wewe ni serikali pale ulipo.na jukumu lako kubwa ni kutiza wajibu wako,MJENGA NCHI NI MWANANCHI MWENYEWE.USIULIZE NCHI ITAKUFANYIA NINI,NINI UMEFANYA KWA NCHI YAKO.(don’t ask what the country can do for you,ask what can you do for your country.)sasa kwa sasa tunaishi dunia tofauti ina mablogs websites hizi ndizo zama za uwazi na ukweli ambazo ndio ilikua mbiu ya serikali awamu ya tatu ambayo nayo ilifanya kazi nzuri sana ya kuendeleza tanzania yetu,kwa mambo mengi mazuri ambayo yanazimika tu kwa dhana mbaya.hivyo kutona na uwazi huu ndugu zangu tumieni uwigo huu wa mitandao na sio kwa kulaumu, kutukana au kukashifu.penye zuri semeni ni zuri na penye marekebisho kosoeni kwa busara.pia elimisha kama prof.mbele alivyowezakufanya tanzania bado changa inahitaji changamoto za watanzania wenyewe ndio tunauchungu na nchi yetu yenye baraka ya kijani,kama ilivyo bendera yetu.

  KUMBUKA VIONGOZI WOTE NI WATU,BINADAMU.NA KUNA MSEMO USEMAO “BINADAMU SI KAMILI”HIVYO KUNAWEZA KUKAWA NA MAPUNGUFU ILA TUSIWANYIME AMANI.
  PIA UKIKOSOA NA KUELIMISHA,KAMA PROF.MBELE.WAKO NAIMANI WANASOMA NAKUFUATILIA MAWAZO NA MAONI YETU WANAWEZA KUJIREKEBISHA NA WAKAFANYA MAZURI YENYE MANUFAA KWA NCHI YETU TANZANZANIA.

  BINADAMU.MZEE MWINYI LIPOMALIZA MUDA WA UONGOZI ALISEMA”MAZURI YOTE YETU SOTE,NA MABAYA YOTE NIMEFANYA PEKE YANGU”.BINADAMU SI KAMILI TUWE NA HURUMA.
  MDAU WASHGTON

 • joshua said:

  i disagree with you… i still think that our president needs to step up the plate differently…. he is full time traveling.. i sometimes wonder how he is giving advises to his subordinates when he is not in the country 100%. I mean i remember when Nyerere was in the office, he traveled but not that much but JK is traveling like crazy, I mean dont you think that its bad as it is to spend poor peoples tax shillings? i saw his pictures with president obama, he was a little bit nervous, and i didn’t understand why… + if he is going to all these big countries to ask for $$ and not ask for ideas then he is embarrassing all of us. Get it together JK.

 • yeremiah said:

  hivi ni katangaza vipi tanzania wakati mie naishi marekani na sijaona kokote imetangazwa ziara yake si CNN, wala local TV za hapa nilipo mpaka nilivyoganlia Michuzi blog ndio nikakuta mambo kibao… kwa kifupi sijaona JK katangazaje nchi yetu zaidi tu ya yeye mwenyewe kuwa nchi tofauti kila ukiangalia habari za nyumbani.

 • Anonymous said:

  Kama ningekuwa nauwezo Prof, ningekurudisha home ukaielimishe jamii hata kwa week moja kwenye luninga. hongera sana msomi mkuu.

 • Mtanzania said:

  Profesa,
  Naomba nipingane nawe.Kwa vile wewe ni msomi,nilitarajia ungeangalia pia upande wa pili wa shilingi,yaani hoja za hao wanaolaumu ziara za JK huko nje.JK ameshakuja Marekani takriban mara 6 sasa,ilhali amekuwa madarakani kwa wastani wa miaka mitatu tu.Hiyo ni sawa na ziara 2 kwa mwaka.Sasa unapotwambia (nakunukuu) “Kwanza, waMarekani kwa ujumla hawazijui nchi za Afrika kwa majina. Sana sana wanajua tu Afrika. Kuja kwa JK daima imekuwa ni fursa nzuri ya waMarekani kuijua na kuikumbuka nchi inayoitwa Tanzania….” ina maana mara ya kwanza hakufanikiwa ktk jukumu hilo ulilopamchika la “KUWAJULISHA WAMAREKANI KUHUSU TANZANIA”,ikabidi aje tena na tena na tena!Hivi ni kazi ya Rais PEKEE kuitambulisha nchi kwa dunia?Ubalozi wa Tanzania Marekani unafanya nini?Bodi ya Utalii je?Trade Centres zilizotapakaa kwenye balozi zetu zina kazi gani?Mbona hatusikii Kagame,Museveni,Kibaki,nk wakiwa kiguu na njia kuja Marekani KUWAJULISHA WAMAREANI KUHUSU NCHI ZAO?

  Pamoja kuwa wewe ni msomi ninayekuheshimu,lakini nadhani uchambuzi wako ni finyu.Unadhani tatizo la Wamarekani kutozielewa majina nchi za Afrika ni kwa vile marais wa nchi hizo hawatembelei huko au ni tabia iliyojengeka miongoni mwa Wamarekani kwamba kuna DUNIA MBILI:Marekani na the rest of the world?Hebu jipe muda wa kuchunguza,sio kuhusu Afrika pekee bali hata Ulaya.Jisumbue kuwadadisi wanafunzi wako kuhusu upeo wao about nini kinachoendelea nje ya Marekani.Zilch!Kwahiyo,hata kama JK angeamua kufungua Ikulu ndogo hapo DC bado isingebadilisha attitude ya Wamarekani kuhusu the world away from the US of A.

  Profesa,hivi kwa usomi wako unadhani kinachofanikisha kuitambulisha nchi ni ziara za viongozi wake au mafanikio ya ndani ya nchi husika?Kagame hakuwa ndani ya watu maarufu duniani 2009 (wa Jarida la TIME) kwa vile anakuja sana huko USA.Pamoja na mapungufu yake,Kagame ameweza kui-transform Rwanda from ashes,kutoka mauaji ya kimbari hadi kuwa miongoni mwa nchi zenye kufanya vizuri katika uchumi.

  Pia Profesa Mbele,kabla ya kukimbilia kusifu ziara za JK including hiyo iliyojumuisha “wafanyabiashara” ungejishughulisha kidogo kufanya assessment ndogo tu ya ziara zilizotangulia.Ngoja nikusaidie kidogo.Neglecting malalamiko kwamba baadhi ya “wafanyabiashara” waliokuwa kwenye msafara wa rais hawakuwa wanafanyabiashara in the real meaning of the word,hatujafahamishwa mafanikio yoyote ya kuwemo kwao kwenye ziara hiyo ya JK.Je unaweza kutuambia ni kampuni ngapi za Kimarekani zimeingia japo ubia na angalau mmoja wa wafanyabiashara hao?ZILCH!

  Tatizo la baadhi wasomi wetu,mnakuwa wepesi kutoa majibu kwenye maswali magumu.Inasikitisha zaidi msomi husika anapokuwa profesa mwenye heshima kubwa kwenye jamii.Badala ya kuangalia faida za ziara hizo hapo Minnessota,kwani usiangalie kwa upana zaidi hadi ukajumuisha Tukuyu,Malampaka,Kemondo Bay,nk?Ziara 6 za JK zimepeleka umeme katika vijiji visivyo na umeme?Zimetatua matatizo ya maji mijini na vijijini?Zimeondoa upungufu wa walimu na vitendea kazi mashuleni?Huo ndio uchambuzi wa kisomi,na sio huo wa kuangalia haiba ya mtu badala ya ufanisi wake.

  Naomba nikunukuu tena: “Watanzania tumezoea kukaa vijiweni na kutoa lawama kwa wengine. Nayachukulia malamiko kuhusu safari za nje za JK kwa msingi huo”.Maneno haya ungetaraji kuyasikia KIJIWENI NA SIO KUTOKA KWA PROFESA.Umeshafanya utafiti wa kukuwezesha kujua idadi ya “Watanzania wanaokaa vijiweni”?Kama watanzania tumezowea kukaa kijiweni,mbona wewe ni profesa huko Marekani?Tuambie siri ya wewe kukaa kijiweni (tukikubaliana na hoja yako) lakini ukafanikiwa kupata uprofesa na sasa uko Marekani!Twafahamu bayana kuwa mkaa kijiweni hawezi kupata mafanikio kama yako.Au mwenzetu si Mtanzania?

  Hapohapo,kama tumezowea kukaa vijiweni,hudhani kwamba tuna haki ya kumlaumu rais wetu anayetukimbia vijiweni na kuja “kula kuku kwa bata” huko mliko akina Profesa Mbele?

  Zaidi ya hapo,kuna watu wataona kama unawatukana unapodai (bila data za kusapoti hoja yako) kuwa watanzania wanapenda kukaa vijiweni.By the way,kuaa vijiweni si dhambi au kosa la jinai.Ni utamaduni wetu tangia enzi za zamani kukutana mahala,kupiga soga,kunywa togwa,ulanzi,au kubadilishana mawazo.Ndio UJAMAA.Mbona hulalamikii baadhi ya Wamarekani (hususan weusi) wanaoendekeza vijiwe in forms of gangs like the Crips,Bloods,nk?Na hivi ni vijiwe vya uhalifu:uporaji,madawa ya kulevya,nk.Lakini tofauti ya vijiwe hivyo na vya Tanzania ni kwamba hatubaguani.Nenda Southern Central LA,utafiti uwezekano wa kukuta kijiwe chenye mchanganyiko wa Whites,Blacks na Latinos!ZILCH!Hao wote si wamarekani?Kumbe basi angalau vijiwe vyetu vina kitu cha kujivunia:muungano pasipo kujali backgrounds zetu.

  Lakini,mie ningependa kukupa changamoto zaidi kuhusiana na hilo hitimisho lako kuwa Watanzania wanapenda kukaa vijiweni.Naelewa unamaanisha nini,japo ilipaswa ufafanue “by kijiweni” unamaanisha nini ili usije leta tafsiri kuwa “uko Mrekani,sasa unadharau ulikokulia”.Unadhani watu wanakaa vijiweni kwa kupenda au mazingira yanawalazimisha kufanya hivyo?Hivi,wakulima wanaotoka mashambani wakiwa hoi bina taaban,huku hawajua kama lini chama cha ushirika kitawalipa fedha za mazao yao ya misimu kadhaa iliyopita,wanafanya kosa kukaa vijiweni “kupunguza mawazo”?Je safari za JK huko Marekani zinawanufaishaje “wakaa vijiweni hawa”?Hap jumuisha walimu wanaosubiri mishahara kwa miezi sita (ilhali shule wanazofundisha hazina madawati),akinamama wanaotembea maili kadhaa kutafuta maji,wamachinga ambao wanatembea umbali mrefu kama JK ,only difference ni kuwa yeye anapaa angani na wamachinga wanatembea kwa mguu.

  Mwisho,ningetegemea Profesa ungetambua kwamba tatizo la Tanzania sio KUTOJULIKANA huko Marekani au kwingineko bali ni viongozi walafi,wabinafsi na mafisadi.JK atakuja huko,”ataitangaza Tanzania mchana na usiku”,halafu kinachopatikana kinaishia kwenye nyumba ndogo za mafisadi.Kwani basi hamkumuuliza KAGODA NI MDUDU GANI?Maana pengine wasomi kama nyie mkiungana na watu wa vijiweni kama sie labda viongozi wetu watafumbuka macho na kujua ahaaa kumbe kelele za ufisadi sio za vijiweni pekee bali hata kwa wasomi kama akina Profesa Mbele!

  Sijui ni matokeo ya hegemony ya TANU na CCM ambapo viongozi walikuwa,na wameendelea kuwa,miungu watu,basi baadhi ya wenzetu wakipata fursa ya kugusana bega na kiongozi wanasahau kabisa mapungufu,uzembe,ubabaishaji,udanganyifu,ufisadi,nk wa viongozi husika.Samahani kama nitakukosea heshima,lakini naamini makala yako hii ni matokeo ya “ugonjwa huo”.Baada ya JK “kutumia haiba na mvuto wake vizuri”,baadhi yenu mmeridhika kabisa kuwa mtu huyu aliyeahidi maisha bora kwa kila Mtanzania wakati anaomba kura 2005,amefanikiwa….well,KUITANGAZA TANZANIA HUKO MAREKANI!

  Kaaazi kwelikweli!

 • Kai said:

  Juzi kiongozi wa waimbaji alisema, watu wa mataifa mbalimbali walete nyimbo zao. Akaendelea kusema “taifa kama la Afrika tutafurahi kupata wimbo kutoka huko”. Nilishangaa. Hapa marekani ndivyo uelewa wa walio wengi ulivyo. Naungana na Prof. Mbele kueleza faida ya watu hawa kuelimishwa. Nchi ya Marekani uelimishaji wake mwingi huegemea katika maandishi. Ikiwa kitu kimeandikwa hupewa heshima. Hivyo Ujio wa Mkuu wa Nchi kama Raisi unapoandikwa, na kisha yale aliyoyasema yakaandikwa, elimu inakuwa na athari kubwa na kwa watu wengi. Walio wengu hapa marekani sio tu hawayajui yanayotokea nje ya Marekani, bali pia wengine hufahamu tu yale ya Jimbo lao. Wala hawana habari ya yanayotokea kwenye majimbo mengine labda kama ni habari ya kusisimua na ikapewa kipaumbele na vyombo vya habari.
  Ninatofautiana na Bw. Joshua Said. Nyerere kutokutembea sana nje ya nchi kulikuwa na sababu zake zilizoendana na hali ya wakati ule. Na hata kukaa sana nchini na kuwatembelea wananchi kulikuwa na maana sana kutokana na wakati ule pia. Kila kitu huenda na wakati. Ukiangalia siasa za wakati wa Nyerere (Vita baridi) mvutano wa pande mbili za mashariki na magharibi, ukaangalia umuhimu wa ujenzi wa nchi changa na kuelimisha watu wa nchi yake kwanza, kila kitu kilikuwa na wakati wake.
  Wakati wa JK, watu wa nje wanahitaji zaidi elimu kuhusu TZ, ili watuone kama watu tunaoweza kushirikiana nao kuleta maendeleo katika dunia.
  Jambo ambalo ninatofautiana kidogo na Prof. Mbele ni kuwa na mawazo niyaitayo ya mjumuisho. Amejumuisha mno kusema: “Watanzania tumezoea kukaa vijiweni na kutoa lawama kwa wengine.” Hapa Prof. amejumuisha mno. Angaliweza kusema: “baadhi ya watanzania…” maana kwa hakika kuna wengi wengine kama yeye ambao hawakai kutoa lawama bali wanatoa michango na mawazo kuleta maendeleo. Wako wanaosema “Watanzania ni wavivu…” hawa hawawatendei haki wale wengine ambao hufanya kazi kwa bidii usiku na mchana. Kuna wachache wavivu, au labda ni wengi, ila sio wote. Hii haitakuwa na tofauti na wale ambao hawajawahi hata kufika nchi yoyote Afrika, wanabaki kusema tu, Waafrika ni wavivu, wanapenda kupigana hovyo, ni wachafu n.k Huku ni kujumuisha mno.
  safari za JK, zina manufaa na sisi wengine wote hauna budi kuziunga mkono na kila mtu afanye juhusi mahali alipo ili kuwaelimisha na kuwakaribisha watu, ili WASHIRIKIANE na Watanzania katika sekta mbalimbali ili kuleta maendeleo.
  Kai
  New Jersey

 • Peter said:

  nashaangaa mtu anajiita profesa kuandika makala yenye uchambuzi wa kiwango cha chini kiasi hiki!!! ana lake jambo huyu wala si kawaida!

 • David Matthew said:

  Dear Prof Mbele,
  It is true in Tanzania as in many third world countries talk a lot about development,about expanding the number of goods and services and the capacity to produce them.Goods Make our lives more useful and easy and happy.So it is very clear by now that all this development is for man and is made by man,you see it always comes back to man.Man is the main purpose of development.Bu Man cannot be developed by another,he can only develop himself,it his ability to work deliberately (in cooperation with others) for a self determined purpose that distinguishes him from another man.This is what development mean.

  Therefore having said that our people needs to be reminded to work tirelesly with their own defined puposes and missions so as to make their lives good.All presidents meet other presidents it is a human nature to meet other people but Tanzanians need to be reminded he will not come back with a stach of bag filled with money.

  Ni hayo tu kwaleo,
  David Matthew,
  Electrical engineer,
  Ohio

 • Yoshua said:

  Kamala, wewe ndiye Lutatinisibwa? mbona siku hizi sioni tena makala zako za utambuzi katika kwanza jamii? zilinielimisha sana ndugu, zikirudi ni vena sana kwangu au umeingia mtini? huwa nanunua gazeti ili nikusome sasa umenitelekeza ndugu au unachimba ili kuja na vitu vizuri zaidi nini?

 • Masalakulangwa said:

  Prof;
  Rudi tu Tanzania ukagombee ubunge na nakupa jimbo songea linaloongozwa na dr feki Nchimbi. Mengi uliyosema hayana faida yeyote na niyakufikirika zaidi. Minnesota Mtalii JK kakutana n Watanzania kama wewe. Je unataka kutuambia nyie hamfahamu Tanzania? Wamarekani anaokutana nao kama huyo balozi ni wazi wanaelewa Tanzania iko wapi. Umeongea na jirani zako kwenye neighborhood yako wakakueleza wameifahamu Tanzania baada ya ujio wa msanii?
  Eti tanzania ina mazingira mazuri ya uwekezaji!!! Mazingira mazuri my black (vulgar). Mazingira mazuri hayaletwi tu na kukosekana kwa miungurumo ya risasi, umeme wa mgao, maji hakuna, miundo mbinu mibovu utafikiri tuko karne ya 10 sasa hayo mzingira mazuri ni yapi?
  Halafu unasema kuwa eti alikuja na wafanyabiashara unachekesha kweli watu wanaokuja kutangaza viatu vya ngozi ya kenge ambavyo havikutengenezwa Tanzania utawaitaje wafanya biashara?
  Kuhusu watanzania kuwa waavivu nako ni kupotoka, hivi watu wa nyanda za juu kusini wanaozalisha mahindi yanaoza kwa sababu tu hakuna miundo mbinu ya kuyafikisha sehemu nyingine za Tanzania utawaitaje wavivu. Watu wanao hangaika kwa mitumbwi ya kasia ziwa Victoria kupata sangara wanaosafirishwa nje ya nchi na kuleta fedha za kigeni hii dharau ya kuwaita wavivu na watu wa vijiweni inatoka wapi?
  Nchi kama Botswana rais wake hatembei tembei kama wa kwetu je ni kweli haifahamiki na ni maskini kuliko ya kwetu?
  Kuomba ni kuomba tu uombe pesa uombe jembe bado ni ombaomba tu! Ziara hizi za msanii JK hazina faida. Rais anakwenda Hollywood halafu eti tuaminishwe kuwa kunafaida. Mimi simo na nasema tena simo.
  Hasara zake ni kuwa kwanza anatumia pesa nyingi mno ujumbe wa watu hamsini ni matumizi mabaya kabisa ya kodi zetu. Kisha hao watu wanafanya shopping halafu wanarudi na vitu ambavyo hawalipii kodi huu ni ufisadi. Pili ni kujilemeza kudhani maendeleo yataletwa na hao anaowatembelea. Wewe profesa uko huko si ndio wanasema hakuna ‘free lunch’ mnapotegemea JK aje kuuuza sura halafu wamarekani wawatambue mnakuwa mnafikiri nini hasa?
  Labda profesa umeahidiwa ubunge na kisha uwaziri ndio maana unaanza kupiga porojo. Sitashangaa maana wasomi wa bongo ndiko mnakokimbilia siku hizi

 • Mzalendo said:

  Prof. unaangalia upande mmoja tu wa shilingi. Unasahau kuwa Marekani haina rafiki wa kudumu. Kwa sasa inamkumbatia JK kwa kuwa anapalilia masilahi yake. Kumbuka siku za nyuma Museveni ndo alikuwa kipenzi chao na baada ya kumaliza kufyonza utamu sasa hawamkumbatii tena. Kwa sasa ulaji uko TZ na baada ya miaka kadhaa watagundua ulaji sehemu nyingine na wataanza kumponda JK na TZ. Yangu macho na masikio!

 • mickey said:

  MBELE, YOU ARE DEAD WRONG.
  Naamini kabisa kuwa ziara za nyingi za nchi nje za kikwete ni
  kuomba misaada na ndio maana nchi imekuwa nyuma miaka yote kwa
  sababu ya kutegemea misaada ambayo kila ushahidi unaonyesha kuwa
  kuwa aina tija especially ile inayokwenda serikalini. nchi yetu
  imepolomoka kiuchumi kwa sababu ya misaada ambayo imewafanya
  viongozi wetu kuacha kukaa chini na wananchi ili kupanga namna
  ya kuinua uchumi wanachukua njia raisi ya kuombaomba. mwaka 1970
  TANZANIA ilikuwa na watu asilimia 11 walikuwa wakiishi chini ya dola
  moja kwa siku leo hii ni ni zaidi ya asilimia 66 ya WATZ wanaishi
  chini ya dola moja kwa siku. prof. mbele hakuna mfanyabiashara wa
  maana atakayesuburi mpaka rais aje marekani ndio aje kutafuta soko
  na pia hakuna mfanyabiashara yeyote wa marekani atakayefanya biashara
  na TANZANIA eti kwa sababu ya kuona sura ya rais, wafanya biashara
  biashara wa marekani wakiona kama kuna uwezekano wa wao kutengeneza
  pesa they don’t care kama wamemwona au vipi watakuja kutengeneza pesa
  na kama wanataka info. kuhusu TZ watakwenda kwenye vyombo usika wakim
  emo CIA na RIPOTI ZA UN KUHUSU MAZINGIRA YA BIASHARA TZ na siyo
  kutoka kwa kikwete kwani wanajua kuwa hawawezi kupata info. ambazo
  ni Independent. kuhusu kutangaza nchi uhitaji rais kutangaza nchi na
  kama ushahidi unao toa nchi gani rais alifanya ziara nyingi za nje
  kuitangaza nchi ikaendelea. faili lako la kibiashara pale UN na CIA
  ndio litakalokutetea tu na vinginevyo.
  kikwete kama anataka TZ iendelee akae chini na kuandaa rasimu ya kuac
  hana na misaada ndani ya miaka 5 hadi 10.
  pili akae na wananchi wa TZ ili apange mikakati ya kuinua uchumi ili
  kuziba pengo litakalotokana na kujitoa kwenye misaada.
  tatu aandae mazingira mazuri ya kibiashara kwa kupunguza viwango
  vya kodi na kukata matumizi mabaya ya pesa zikiwemo safari za viongoz
  i za nje zisizo na tija yeyote na pia swala la ufisaji.
  aandae mazingira mazuri ya kuweka FOREIGN DIRECT INVESTMENT NDANI
  ya TZ na siyo kupewa pesa viongozi wa TZ kama kikwete na chenge.
  Waandae mazingira ya kuwasaidia wafanyabiashara wadogo na wakulima
  kwa kupitia microfinance. nchi lazima itainuka kwa watu kuwezeshwa
  kunyanyuka wenyewe ili kukuza uchumi wao na siyo kupitia misaada ya
  kutoka marekani ambayo imekuwa ikimfanya kikwete kuwajibika sana
  kwa worldbank na IMF kwa kuwasikiliza wao kutuambia nini cha kufanya
  ili tuendelee kama watoto wadogo. imefika wakati kwa VIONGOZI kuacha
  uvivu wa kufikiria na kukaa nyumbani na kuinua nchi zao.

 • Masalakulangwa said:

  Hili gazeti inabidi mliite mwisho jamii badala ya kwanza jamii. Sababu yake nikuwa hamtaki kupingwa. Maoni yoyote yanayopingana na mwandishi wa makala basi hayana nafasi. Karne za kulishwa kila kitu zimeshapita. Nilitoa maoni yangu kupinga na Mbele lakini kwa sababu nilipingana naye yalikaa kama dakika tano za nyie kusoma nakuyafuta. Kila la kheri na kigazeti chenu. Lakini kuna msemo mmoja wa busara; “kama watu wawili wakiwa na mawazo yanayofanana basi mmoja wapo hatakiwi kuwepo.”

  Masalakulangwa,
  Nyamadoke, Sengerema, Tanzania

 • Sagamba Tumaini said:

  Dear Prof. Mbele, nakupongeza sana kwa maoni yako hayo kwani hapa kwetu Tanzania hasa kwenye miji mikubwa kama Dar,Arusha, Mwanza na kwingineko hayo ni mazungumzo ya kawaida hasa kenye vijiwe vya kahawa na kucheza bao, utakuta watu wanaongea kwa mitazamo yao na kujifanya wao wanajua kila kitu kumbe sio kweli kwani hata kazi zao wanashindwa kuzifanya, na kujifanya wao ni mahodari sana wa kumpangia kazi na majukumu Rais,Nawaomba Watanzania wenzangu tuache maneno na majungu tushirikiane na Rais na viongozi wetu wengine kufanya kazi tujenge nchi yetu.

  Ni mimi mdau wa KIMARA TEMBONI
  DAR,

 • kamala said:

  Yoshua, sina jibu ndg. tunakatazwa kutoa vitu hasi!

 • kamala said:

  Yoshua, sina jibu ndg. labda jitambue litazaliwa upya!

 • Juma Mkwalla said:

  Prof.Mbelle jua kuwa Tanzania ina Serikali,ambayo ni Chombo ghali sana
  kwa Nchi Maskini kama Tanzania.Mbele acha kujikomba kwa JK ukitegemea
  ulaji ujapo amua kurudi Tanzania.Tanzania ina watendaji wake wakiwemo
  wataalamu wa Masoko na Wachumi tuwalipao kwa kazi ambazo huyu JK kila
  kukicha anaota kwenda nje kuinadi Tanzania.Nionavyo Mimi JK ni Kuadi wa Soko huria ambalo halimuhitaji Rais wa Nchi kulitangaza.

 • jumbe said:

  well mimi sikubaliani na professa and especially watu wanaotumia tittle zao as validation kwa vitu wanavyosema, in my opinion naona professa haelewi mtazamo wa nchi amekuwa excited kuona jk kapata attention minnisota wakati nchi yetu inadidimizwa na mafisadi, hivi professa unajua state of minnesota imekumbwa na recession, kama most states? hata budget yake iko kwenye deficit, sasa biashara na wananchi wa minesota wanumia na hali ya uchumi ilivyo sasa hivi wakati wewe unashangilia eti kikwete kapewa digrii ya heshima embu niambia hiyo digrii inamsaidiaje mtanzania ambaye anakula mlo mmoja kwa siku, hivi gharama za safari za kikwete na entourage yake yote mpaka sasa imefikia wapi? i bet his last trip to us imetucost walipa kodi at least 300,000$ and i mean at least! anafanya hizi trip all the time, hivi sisi watanzania huo uwezo tumeutoa wapi? nalia kuwaona kina mama wanaenda hospitali wanaambiwa hawawezi kupata matibabu kwa sababu hawana uwezo, mgao wa umeme… and many more haya mambo raisi angekuwa nnchini kuyasimamia mwenyewe badala ya kuzurura huku watu wanaharibu and eti tunawablame kina lowasa, haya yote raisi ameshayaona lakini bado anazurura zurura eti kuitangaza nchi kwani imekuwa mashindano ya uzuri???

 • Ramadhani Iddi said:

  JK ajue kuwa ana Waziri na Katibu Mkuu Mambo ya Nje.

 • JB said:

  Mlowezi hasitahili kabisa kuongelea Tanzania yetu
  Huyu profesa ni msaliti na watanzania tusipokuwa makini tutapotoshwa sana
  Kodi zetu zinatumiwa ovyo , lakini hawa akina profesa hawajui tunaumia vipi tumuuliza yeye anachangia nini kwenye pato letu la taifa??

  Profesa tunakuheshimu kama mtanzania mlowezi wa marekani achana na watanzania wazalendo , marekani ijue na uendelee kuijua na si Tanzania yetu , Wananchi tunachapa kazi ila viongozi wabovu na watanzania wachache waovu na wasiopenda kwao wanapotosha ukweli

  Let us have a self determination for our success

  Nina Imani ipo siku tutapata kiongozi wa nchi , wapo akina Magufuli wanakuja wataokoa tu jahazi Mungu atawainua ingawaje wanabaniwa

  Ni aibu na nyie watanzania mnaojifanya ati Profesa kawafungua vichwa ni ujinga mkubwa acheni hizo

  Hawa akina Mbele ndo kama akina Collins wa enzi za Bush(mbwa wa tajiri)

  Tujenge Tanzania Rais wetu tulia na uchape kazi mbona ulianza vizuri JK

 • Mama Kitindi said:

  Kwanza nimpongeze Prof. kwa maoni yake ingawa natofautiana naye. Suala la kutangaza nchi si muhimu kama kujenga uwezo wa ndani. Hata kama atazunguka dunia nzima kuieleza dunia kuwa kuna nchi inaitwa Tanzania, haiwezi kusaidia kitu kama nchi itaendelea kuwa masikini. Hivi Prof. ni mwekezaji gani wa maana atawekeza nchi ambayo haina barabara nzuri, hakuna maji ya uhakika, hakuna umeme wa uhakika, watu masikini (hakuna soko la ndani), nchi imezungukwa na viinchi masikini vyenye vita, hakuna soko, watu wavivu, njaa kila mahali, ufisadi ndiyo usiseme n.k. Hivi Prof. nani anaitangaza China leo, si inajitangaza yenyewe? Nadhani unakumbuka ule msemo wetu kuwa chema kinajiuza na kibaya……..

  Pamoja na kuwa wengi hawaifahamu vizuri Afrika, lakini wengi wanafahamu kuwa kuna Afrika Kusini, wanajua, wanafahamu kuwa kuna Nigeria (pamoja na uchumi, mpira)na baadhi ya nchi chache za Afrika.

  Tatizo kubwa ni umasikini na matumizi mabaya ya rasilimali, kama tukifanikiwa kujenga uchumi, kukawa na miundo mbinu mizuri pamoja na soko, wawekezaji watakuja tu. Hivyo basi mimi naona si sahihi kwa Rais kila siku kutangaza nchi, anapaswa kuhangaika kuijenga nchi ili ijitangaze yenyewe.

  Nakutakia mema Prof.

 • Joseph Mbele said:

  Kwa kiasi fulani, mada hii inagusia masuala ya utandawazi na maendeleo, na napenda kuwakaribisha wanaotaka kulumbana nami, siku nzima, ana kwa ana, kwenye warsha nitakayoendesha Tanga tarehe 29 Agosti 2009, kama ilivyotangazwa hapa.

  Kila la heri

 • Yassin said:

  inafurahisha kuona watu wanatoa mawazo yao ila inapendeza yakiwa yakistaarabu basi.

 • bwenge said:

  sikupata wasaa wa kusoma makala hii ilipotoka. prof mbele ninaomba kutofautiana nawe. ufafanuzi wako hautofautiani sana na wa ki-ccm. watu wanaopinga safari nyingi za rais jk wanaangalia gharama (fedha na muda) na faida inayotokana na gharama hiyo. sijui kama unaweza kutupa data za kuthibitisha kuwa safari za jk zina faida maradufu kuliko ambavyo angekuja waziri wa utalii au wa mambo ya nchi za nje kutangaza tanzania. kazi kuu ya rais si kutangaza nchi bali ni kuongoza nchi. hatujamsikia mwai kibaki akizurura au museveni akizunguka kutangaza uganda, lakini uchumi wa uganda unapaa, na sisi tanzania tumebakia kusubiri nani anaingia ikulu ya marekani ili tujipendekeze tupate misaada.

 • Joseph Mbele said:

  Wanaosema ziara za JK nchi za nje hazina manufaa yoyote wasidhani kuwa wanachosema wao ndio kauli ya mwisho. Soma hapa <a href=”http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=2782″

 • Markus Honorius said:

  Maendeleo ni nini? Nani anawajibika kuleta maendeleo yetu?
  kuna hesabu hii: “0-1 au i-0?”.
  Nipo mawazoni ndiyo maana nawauliza swali la hesabu hiyo. Tujadili

  Upanga west, Dar Es Salaam, Tanzania

 • ludete J said:

  Jk ni sehemu ya kazi zake kusafiri nje ya nchi kadri anavyoona inamanufaa kwa wa-Tanzania. Tatizo kubwa la wananchi wa Tanzania ni kufanya politiki na kusahau kuwa kaziya Serikali ni kutengeneza mazingira ya mtu kujiletea maendeleo.Kuna bwana mzungu mmoja aliwahi kuniambia,umaskini wa mtu uko kichwani,akatoa mfano kwamba wanyang’anye mali matajiri wote na uzigawe upya kwa watu wote:baada ya muda fulani,waliokuwa matajiri kwanza watarudi kuwa matajiri na maskini watarudi kuwa maskini.Hivyo,MH.KIKWETE anajenga mazingira kwa watanzania na nijukumu lao kutumia fursa hizo.

  Kukaa kijiweni na kupiga porojo bila kufanya kazi na lawama kumtupia rais wa nchi ni kutafuta visingizio tu.Namuunga mkono Pof.

  Ludete,Moshi

 • Joseph L. Mbele said:

  Nilitoa tangazo kuwa nakuja Tanzania kuendesha semina, nikawaalika wote ambao wangekuwa tayari kukabiliana nami ana kwa ana, kwa hoja. Nilitoa tangazo na mwaliko huu kutokana na kauli nyingi zilizotolewa hapo juu. Nilifika Tanga, nikafanya semina na Dar es Salaam pia, na zote zilitangazwa, na hii ya Dar ilitangazwa hadi kwa Michuzi, tarehe 4 Septemba. Lakini jamaa sikuwaona. Katika warsha hizi, tulikuwa na muda wa kutosha wa mapumziko, ambao hao jamaa wangeweza kunikabili. Lakini sikuwaona. Inakuwaje kuwa walishindwa hata kutuma watu, iwe ni waandishi wa habari au marafiki? Nawajibika kuwashangaa. Nitaendelea kuja Tanzania, kuendesha hizi warsha, na nitawategemea hao jamaa waje. Vinginevyo nitaendelea kuwashangaa. Kuona taarifa za warsha nilizofanya mwaka huu, bofya hapa.

 • halfan said:

  Mimi kwa mtazamo wangu ni kwamba tumempata rais ambae anapenda sana kuomba. Ukizingatia hata upatikanaji wa urais wake aliomba pesa Uarabuni na ndio chanzo ya yote haya ya Dowans, Na panga pangua huyu rais hawezi kukubali huyu shemeji yake yaani Rostam ahojiwe au awekwe ndani kwani kwa kufanya ivyo. Anajua fika shemeji yake atamuumbua. Kuna siri kubwa kati yao. Turudi kwenye mada ni rais gani asietaka kutulia nyumbani kwake angalau akatatua matatizo ya nch yake. Mawaziri wake wanaboronga lakini hakuna hatua yoyote anayochukua ndio maana wanamdharau hawafanyi kazi kwa vile niwanamtandao hata ukifanya kosa hakuna atakae kuondoa. Ni muda wake wa kukaa nchini na kutatua matatizo kama haya achane na wanamtandao. Inavyoonekana rais wetu anaogopa kukaa nchini kwasababu ya hawa watendaji wake anaona bora azunguke siku ziende. Kwani kuna misafara mingine ambayo apashwi yeye kwenda na sio kwamba huwa anaalikwa inavyoonekana ni yeye anaeomba mialiko ili awatembelee.
  Asante
  N.I

 • karubandika said:

  Sasa Mmarekani unayeishi naye na kumfundisha akijua kuna Tanzania tunanufaika vipi?

 • Joseph L. Mbele said:

  Nawaarifu wote wanaothamini mijadala kuwa nimechapisha kitabu, ambacho kimezama zaidi katika kuelezea mtazamo wangu. Kinaitwa CHANGAMOTO, na kinapatikana hapa

 • Bramo said:

  Proff it seems you know nothing about our country Tanzania, its shame for an educated figure like you kushabikia mambo ambayo kimsingi hayana manufaa kwa nchi yetu.
  Naomba nitofautiane na wewe kama ifuatavyo
  (1) Nchi haijulikan tu kwa Rais kutembea tembea,thats why Marekani wana balozi wao hapa,have you seen your pointless..
  (2)Hatukatai kuwa safar zake hazina mafanikio,lakini ulikuwa wapi hadi uibbuke na hoja zako katika kipindi hiki karibu na uchaguzi(kuna mtu amesema anahisi unajipendekeza kwa Rais ili one day akukumbuke kwenye ualme wako)
  (3)Suala la nchi kufahamika kimataifa,linategemea sera na mipango ya nchi,hasa hasa kwenye rasilimali za nchi,Tanzania inafahamika kwa hilo coz ina sera mbaya zinazowanufaisha hao unaotaka waijue nchi yetu.
  Mwisho kabisa sisi watanzania tunaokaa nchini kwetu ndo tunaoathirIWA Na maoni ya watu kama nyie,nakushauri ukae kimya huko huko marekani na utuachie mambo yetu ya ndani,kama ungekuwa na uchungu na nchi yetu ungerudi hapa nchini kuja kufundisha

  Bramo
  Computer and Information Technolgy Engineer

 • Joseph L Mbele said:

  Bramo, tarehe 3 Julai, mwaka huu, nitaendesha warsha Arusha, kuhusu Utamaduni na Utandawazi. Semina itafanyika katika ukumbi wa Arusha Community Church, kuanzia saa 4 asubuhi, hadi saa 7 mchana.

  Njoo au waambie marafiki zako waje, ili kuthibitisha kama kweli mimi sijui chochote kuhusu Tanzania, kama unavyodai.

  Vile vile, baadhi ya vitabu vyangu vinapatikana hapa Dar, simu namba 0717 413 073 na 0754 888 647. Nendeni mkavinunue, mvisome, halafu uone kama hayo madai yako yana msingi.

  Unanishangaza unapotoa sifa kwa waTanzania tunaokaa nchini kwetu, kama vile hiki ndicho kigezo cha uzalendo. Pamoja na waTanzania wazalendo hapa nchini, kuna pia mafisadi na wahujumu wengi hapo hapo. Kama hukujua hilo, basi ujiulize kama wewe nawe unaijua kweli Tanzania au ni mbambaishaji.

 • Tony kabetha said:

  Prof:Mbele,
  Mtazamo wako na hoja zako zinawakirisha fikra ulizonazo na unazo dhani ni sahihi, lakini upo wrong, huna mvuto na unaongea ki- ushabiki tuu, hakuna mtu wa maana anaweza krupoteza muda wa kukusikiliza.

  Mawazo na majibu unayo andika yangekuwa na maana sana kukiko uso kwa uso tumekupa muda wa kujiandaa na kuandika bado umetoa pumba tupu kuhusu safari za Rais.

  Prof.kama wewe ni hatari kuliko kifua kikuu kwa Nchi kama Tanzania, kwa sababu huna mbinu mpya. Rejea hoja za prof. Bwenge na vijana wengi hapo juu utaelemishwa for free. Umetoa hoja ya uraia mbili unaonekana ama huji unachosema au hutaki kuelemika.Unaongealea kutangaza Nchi na biashara kwa kusafiri katika karne hii ya Network and technology? I’do question your credibility.

  Tony kabetha/New York

 • Maria David said:

  Ni kweli safari za rais wetu sasa zimezidi maana zingine hazimfai kabisa lakini bora asafiri tu.Mfano zingine zinamhusu waziri husika lakini utakuta anaenda yeye au wakati mwingine wanaenda wote na waziri wake sasa hapo yeye anakwenda kufanya nini kama si kutembea na kuacha masuala ya msingi hapa nchini.Kwanza hii ni ghalama katika nchi ambayo raia wake bado wanatawaliwa na umasikini wa hali ya juu. Mimi sikubaliani kabisa na eti safari zake ni katika kuomba misaada huko nje.Prof. kweli wewe unaweza kuwa baba wa nyumba kwa kutegemea pesa za jirani yako.Sasa kwa nini sisi watanzania tutegemee misaada zaidi kwa maendeleo ya nchi yetu. Ndio maana watu wetu bado wanaendelea kuwa masikini kila kukicha. Migomo kila upande katika nchi iliyojaa neema kila mahali. Kama nchi nyingine zinaendelea kwa kuuza maua tu kwa nini sisi wenye kila rasilimali kama madini,mifugo,utalii,ardhi nzuri yenye mabonde na mito ianyotililisha maji mwaka mzima, watu wenye nguvu za kufanya kazi ambao wamebaki kuzurura ovyo mijini kwa sababu uongozi mbovu wa viongozi wa Tanzania.Tuna wizara za kilimo na masoka zinafanya kazi gani kuleta maendeleo kwa watanzania. ni bora zikavyunjwa kupunguza gharama katika serikali maana haziwalibiki kabisa badala yake rais wetu anapitia nchi za watu kuomba uwekezaji,kwani raia wake wameshindwa kufanya hivyo vinavyoitiwa uwekezaji. Wapatie vijana nyenzo za kufanyia kazi kama matrekta na watafutiwe masoko ya bidhaa zao nchi itaendelea. Cha kustaajabu leo Rwanda ambayo imepigana vita takribani miaka 20 imeshatupita kwa maendeleo na rais wao hana safari za kila wakati nje,hivi kweli viongozi wetu hawaoni aibu? inasikitisha sana tutakuwa masikini mpaka lini? halafu viongozi wetu kila kukicha wako na safari nje ya nchi hasa rais wetu amezidi jamani hiyo pes anayosafiria si bora angeitoa kwenye mahospitali yetu ambayo hayana madawa na mashule.

 • Amani Amani said:

  Ndiyo maana kila nikikaa huwa nawadharau sana Wasomi wa aina hii………Sifikiri kama huyu jamaa anaejiita Prof Yuko salama kisaikolojia,na kama yuko salama basi ujue uwezo wake wa kufikiri umefikia kikomo!.Nimemdharau kuliko Mtanzania yeyote.

 • mtweve,Joe said:

  Prof,

  Nimechelewa sana kuisoma hii makala,lakini nakushauri profesa rudi home
  uje ufanye utafiti wa kutosha nahisi ulitoka muda mrefu sana nyumbani,
  na utakusaidia sana huko mbeleni.labda Prof,ungenisaidia kujua ww ni mzaliwa wa wilaya gani hapa tz.labda ningeweza kukusaidia kwa siku nyingine.

 • Ritchie said:

  Hi Profesa Mbele

  Je unaweza kutuambia ni fedha kiasi gani za nchi zinatumika ktk ziara hizo za JK kwa mwaka na fedha hizo zisingekuwa bora kupata matumizi mengine kitaifa zaidi ya hizo safiri? Ni bora tujilinganishe na Uganda na Kenya ktk kufanya matumizi bora. Rais Museveni graduate wa Dar University na anafanya maamuzi ya uhakika nchi yake inaenda mbele kwa kasi inayotalajiwa wale wabovu tunaowafukuza kazi kwa chuki anawachukua na baadaye tunaenda kwake Museveni kujifunza mbinu bora za uongozi huoni aibu kwa kuandika makala ya kipumbavu kiasi hicho na wakati wewe ni profesa ? Museveni hajiadhiri kwa kuwa omba omba na nchi yake inafanya mambo safi basi ni bora profesa urudi bongo ukajenge miundo mbinu ya kuwa omba omba kitu Mwl Nyerere alisha apa kuwa ni utumwa wa fikara na wewe profesa unakumbatia ufukara huo, hongera sana sana

 • malkiory said:

  Profesa, unafanya nini Marekani? kama siyo njaa imekukimbiza. Mimi siwezi kununua kitabu chako kwa kuzingatia hii article yako. Nilikuwa nikikuheshimu lakini kwa hili la kutetea safari za raisi nitasema umefilisika kimawazo na unazeeka vibaya. Wewe hujui kabisa mateso wanayopata watanzani, mateso ambayo yanatokana umasikini ambao chanzo chake ni sera mbovu za CCM.

  Mwisho nataka nikuambie acha kujikomba kwa rais, kama unaompango wa kurudi nyumbani rudi lakini si kwa njia yahii ya kujikomba.

 • malkiory said:

  Profesa mzima huna hata aibu kusema rais ana MVUTO!!!!!!!!!!!!!!! lazima ukiri kuwa umewakosea watanzania kwa hili, hujawatendea haki hata kidogo. Karne ya ishirini na moja, msomi kama wewe utawezaje kujenga dhana dhaifu kama hii. Unawachambua viongozi kulingana na sura na mwenekano wao badala ya kuwachambua kulingana na sera na umakini wao.

 • Joseph Mbele said:

  Kweli umbumbumbu katika Tanzania unazidi kuota mizizi na kuenea. Maoni mengi yaliyotolewa hapa juu yanathibitisha hilo. Yeyote aliyesoma historia ya mahusiano baina ya nchi kama yetu na nchi zile zilizokuwa zimetutawala anafahamu kuwa utajiri wa nchi zile umetokana kwa kiasi kikibwa na historia ya unyonyaji tuliofanyiwa. Waandishi kama Kwame Nkrumah na Walter Rodney wametueleza hivyo. Kwa mfano kama mtu umesoma kitabu cha Rodney, How Europe Underdeveloped Africa, huwezi kuja na hii dhana ya kipuuzi kuwa J.K. ni omba omba. Aende akaombe nini iwapo mali yetu ndiyo iliyojenga uchumi wa huko ughaibuni?

  Wenye kufahamu mambo wanapigania suala la fidia, kwa ki-Ingereza hii ni dhana ya “reparations.” Lakini mbumbumbu walioandika hapo juu hawana habari hiyo. Ukweli ni kuwa hata nchi za ughaibuni zikimpa JK milioni ngapi katika safari zake, hii haiwezi kuitwa msaada, au omba omba. Ni haki yetu kuzishinikiza hizo nchi za ughaibuni zifanye yale ambayo yameshatambuliwa na Umoja wa Mataifa, yaani pesa za kutuwezesha kusonga mbele. Umoja wa Mataifa umetambua hilo, lakini mbumbumbu wa Tanzania hawana habari. Jielimisheni, sio mnakuja hapa na kuleta porojo kama vile tuko kwenye kilabu cha kangara.

  Hao walioandika hapa juu kwa kejeli kuwa ninajiita profesa ni wavivu. Ndio maana hata hawajui chochote kuhusu utafiti na maandishi yangu, ambayo yameufanya ulimwengu wa taaluma kuniweka kwenye hiki kiwango cha uprofesa. Kama hamjui, fanyeni bidii kujielimisha. Msilete porojo hapa. Hata mkapiga kelele kiasi gani, chati yangu katika ulimwengu wa taaluma itaendelea kupanda, kwani naendelea na utafiti, ufundishaji na uandishi.

  Na huyu anayejigamba kuwa hatasoma vitabu vyangu, namtakia kila la heri. Azunguke kwenye vyuo mbali mbali Marekani, ughaibuni, na hata kwenye vyuo vikuu mbali mbali vya Tanzania, atakuta watu wanasoma na kutafakari maandishi yangu. Kama nilivyosema hapo mwanzo, Tanzania tuna tatizo kubwa na kushamiri kwa umbumbumbu, na ushahidi unaonekana kwenye maoni mengi yaliyoandikwa hapa juu.

  Kwa kumalizia, kwa nini watu mnajificha, msijitambulishe? Ni tabia ya woga au kutojiamini? Mwaka huu, nimekaa hapa Tanzania kwa miezi miwili na kidogo, nikiwa nimetangaza kuwa nitaendesha semina katika miji mbali mbali. Nilitangaza wazi na hata kwenye blogu ya Michuzi ilitangazwa. Nilitaka hao wanaopiga kelele waje tukutane ana kwa ana. Kwa mara nyingine tena, kama vile mwaka jana, sikuwaona. Nina haki ya kuwashutumu, kwa sababu wamethibisha kuwa ni wababaishaji ambao hawana ubavu wa kujitokeza hadharani. Nina haki ya kuwashutumu.

 • Joseph Mbele said:

  Wewe unayejiita Melkiori ni mfano hai wa huu uvivu nilioongelea hapa juu. Hujui habari zangu, niliendaje Marekani, na nafanya nini huku, na kadhalika, lakini unakuja hapa na kupiga porojo kama vile unajua.

  Vile vile, unashangaa dhana ya mvuto. Fanya bidii kujielimisha. Labda utafanikiwa kuielewa dhana inayojulikana kwa ki-Ingereza kama “soft diplomacy.” Na labda ukijibidisha zaidi, utaweza kuielewa dhana ya aina mbali mbali za “intelligence,” hasa dhana ya “emotional intelligence.” Zote hizo zinaendana na dhana ya mvuto niliyoileta katika makala yangu.

  Lakini wewe, badala ya kujitambua kuwa hujui, badala ya kuuliza ili uelezwe, unakuja hapa na kujifanya unajua. Unafikiri kuwa mvuto ninaoongelea ni suala la sura. Fanya hima kajielimishe.

  Vile vile, usidhani kuwa makala hizi za Kwanza Jamii ziliandikwa kwa namna ile ile tunayoandika makala za kitaaluma. Ni makala fupi za kuanzisha mjadala, wala si matokeo ya utafiti. Ila watu kama wewe hamna upeo wa kutambua hilo, na ndio maana mnadhani kiwango cha profesa kinaweza kupimwa kwa makala za aina hiyo.

  Dalili moja ya kuelimika na kuwa na ile shauku ya kujifunza na kuelewa yale ambayo mtu huelewi. Mnngekuwa ni watu mnaothamini elimu, mngekuwa na duku duku ya kusoma hiki kitabu nilichokitaja. Mimi nikiambiwa kuwa kuna kitabu fulani

  Kama kuna yeyote anayedhani ninajikomba kwa kiongozi au mtu mwingine yeyote, asome hiki kitabu, sio kuleta hadithi za kubuniwa kama hizi mnazoleta hapa.

 • malkiory said:

  Napingana na wewe Professa Mbele. Kuna nchi nyingine za Ughaibuni hazijawahi kutawala bali wao ndiyo wametawaliwa. Mfano hai ni nchi ninayoishi ya Finland. Right now Finland is the most properous country in the whole world. Maendeleo yao hayajatokana na wao kuwa omba omba, kama sisi watanzania.

 • KISHA BENY said:

  Uchambuzi wa prof. Mbelle hauna umakini kabisi ,anatakiwa atambue kuwa Tanzania itajengwa na watanzania wenyewe. Mfano mzuri nchi ndogo sana SINGAPORE. It is a countr that import most of its needs but now it is very rich compare to Tanzania which depends on donors. I think prof should serously review your presentation because it lacks scientifis data. kwa kifupi tunapoongelea omba omba haina tofauti na wale watoto na wazazi wao tunaowaona kwenye barabara za jijini Dar es salaam

 • Boza said:

  Huna hoja Profesa !

 • Joseph said:

  Ndugu Malkiory

  Fuata ushauri wangu. Fanya juhudi kuejielimisha. Inanishangaza jinsi unavyoongelea Finland, na kujaribu kuiondoa kwenye orodha ya nchi zilizopora mali huku kwetu.

  Nilisema ujielimishe kuhusu historia ya mahusiano baina ya nchi kama yetu na hizo nchi zenye nguvu za ughaibuni. Ni wazi kuwa kuna nchi zilizojitwalia makoloni, zikatawala, kama vile Uingereza, Ufaransa, na Ujerumani.

  Lakini historia haiishii hapo. Kuna suala la ukoloni mambo leo. Na kama ungezingatia ushauri niliotoa pale mwanzo, kwamba upitie maandishi ya watu kama Nkrumah, ungepata mwanga kidogo. Inaonekana huelewi kitu kinachoitwa ukoloni mambo leo.

  Unasema unaishi Finland. Sawa. Nikupe fununu kidogo, kwa kutumia mfano moja rahisi.

  Je, umewahi kusikia kuwa kampuni ya simu (“cellphone”) ya Nokia makao yake ni hapo Finland? Na je, unafahamu kuwa hizi “cellphone” zinatumia madini yaitwayo “coltan” na kwamba madini hayo yanapatikana Kongo, na kwamba habari ya madini, silaha na vita, ndio janga ambalo limeikumba Kongo kwa miaka mingi sana? Makampuni kama Nokia yanahusika moja kwa moja na unyonyaji na uharamia unaoendelea Kongo.

  Kajielimishe kidogo kuhusu suala la madini, kama vile almasi, dhahabu, coltan, uranium, na jinsi ukoloni mamboleo unavyoendelea kwa kutumia sekta hiyo.

  Kwa kifupi, kampuni hii ya Finland inashiriki kikamilifu katika hii hujuma inayoendelea Kongo. Punguza hizi hadithi zako, na badala yake fanya bidii kujielimisha. Hii ndoto yako ya kuitenganisha Finland na historia na mfumo huu inanishangaza.

  Nimetoa mfano moja tu. Lakini kama utaanza kuwa na mwamko wa kujielimisha, utagundua kuwa mfumo wa kibepari wa leo (“imperialism”) ni mfumo unaounganisha makampuni, mabenki, mashirika mengine ya fedha, na taasisi nyingine nyingi, sehemu mbali mbali za dunia. Hii si habari mpya; imefahamika na watafiti tangu zamani sana. Utaiona, kwa mfano katika maandishi ya akina Karl Marx, mwaka 1848. Si habari mpya, na hata hao akina Nkrumah wameikuta na kuiendeleza. Lakini, soma angalau maandishi machache, ndipo uje kuongea hapa.

 • Anonymous said:

  Africa haiwezi kuendelea kwa kutegemea misaada ya nchi za nje. Rais angewekeza kwanza katika kuboresha miundombinu na mazingira mengine ya uwekezaji hasa wa ndani kabla ya kusafiri nje kila siku akitembeza bakuli la kuombaomba misaada. Huu umatonya hautatufikisha popote.

 • DOTTO said:

  Prof….

  Sio kuwa watanzania hawajui umuhimu wa safari anazoweza fanya Rais wa nchi. Tatizo ni ziko ngapi ukilinganisha na Maraisi wengine wa East Africa? Halafu zimekuwa na manufaa gani kwa taifa? Vyandarua? Kondom?ARV? Kwa msaada wa watu wa USA?. Tuache utani JK anatafuta Per diem za kujinufaisha yeye na familia yake na wajanja wanaomuandalia safari hizo. Akae atulie namna gani anaweza kuwasaidia watanzania wake sio kuzurura ovyo tu!! Mara na wanamuziki wa marekani!! mara kuileta Real Mardrid!! Huu ni utani na hafai kabisa!! Watanzania wamepigika ukichukulia kuwa hawana tena moral na utaifa wao. Hii yote ni kutangaziwa kuwa nchi yetu ni masikini kwa takribani miaka 49 tangia uhuru; huku wajanja serikalini na CCM wakichota wanavyotaka kupitia Mikataba ya kinyonyaji na hao unaosema Wazungu wasiotujua. Ni hatari kusema wazungu hawatujui wakati ndio wenye migodi mikubwa Tanzania. Sana sana utuambie Jk amekuwa akienda kupata fungu lake kutokana na mikataba aliyosaini yeye akiwa waziri wa madini!! Prof.Funguka macho sisi watanzania hatutaki utani juu ya hoja hafifu zinazowapendelea hawa wanyonyaji!!!

 • Baba Myonge said:

  Yeye Mheshimiwa anaweza kuvinjali tani yake maana nae ni zamu yake. Ila mimi ninaombi moja kwake “Wamarekani sio watu wa kuchezea, hawana urafiki, suku moja utayakumbuku yangu” ni hayo tu.