Home » Featured, makala

Kamati ya Dk. Wilbroad Slaa yalamba posho mara mbili

12 May 2009 1,418 views 5 Comments

Na Mwandishi Wetu

MAELEZO yalivowahi kutolewa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU), Dk. Edward Hosea, kwamba wapo baadhi ya wabunge wanaopokea posho mara mbili, yamethibitishwa katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh.
Ripoti hiyo ya CAG inathibitisha hali hiyo kutokana na ukaguzi wa hesabu za Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga, mkoani Rukwa, ikidhihirika kuwa malipo yaliyofanywa kupitia vocha ya malipo yenye namba 1/8/066145, yaliyosainiwa na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo yalitumika kulipa wabunge posho.
Katika hali ya kawaida, wabunge hulipwa posho na ofisi ya Bunge hususan wanapokuwa katika shughuli za kawaida zinazohusiana na kamati za Bunge.
“Katika ukaguzi tulioufanya tuliweza kubaini matumizi yasiyostahili yenye thamani ya Sh 8,472,200 ambayo yasingeweza stahili kulipwa kwa kutumia fedha za miradi ya TASAF,” anasema CAG kupitia ripoti yake ya ukaguzi kwa mwaka ulioshia Juni 30, mwaka 2008, ripoti ambayo hata hivyo imekwishawasilishwa bungeni.
Maelezo yaliyotolewa kwa CAG kuhusu malipo hayo yanasema; “Posho kwa ajili ya vikao vya kamati ya Bunge ya hesabu za serikali za mitaa Agosti 7 hadi 16 mwaka 2007 yalikuwa Sh 1,050,000.
Kutokana na kubainika kwa hali hiyo huenda hadhi ya wajumbe wa kamati hiyo inayoongozwa na Dk. Wilbroad Slaa, Mbunge wa Karatu, ikaingia doa mbele ya umma wa Watanzania.
Aprili 2, mwaka huu, Dk. Hosea aliwaeleza wabunge waliojaribu kuhoji uhalali wake wa kuiongoza TAKUKURU wakati akiwa anakabiliwa na tuhuma za kusafisha kashfa ya zabuni ya mitambo ya kuzalisha umeme wa dharura ya Richmond, kuwa kama watafanya hivyo basi nao pia wawe tayari kusikia kashfa zao mbele ya umma. Mara baada ya kutoa kitisho hicho kwa wabunge wakati wa semina ya miundombinu ya uadilifu iliyoandaliwa na Takukuru na Chama cha Wabunge wa Afrika (APNAC) na kufanyika kwenye Hoteli ya Whitesands, jijini Dar es salaam, Dk. Hosea alijikuta katika wakati mgumu.
“Inakuwaje wakati wa mjadala wa Richmond, wewe mkururugenzi wa Takukuru ulikanusha kuwapo rushwa na uchunguzi wa kamati ya Bunge ulibaini kuwepo rushwa ndani ya kampuni hiyo?
Je ni nani mwenye dhamana ya kukuadhibu wewe na taasisi yako kuhusu rushwa’’ alihoji Mbunge wa Busega, Dk.Raphael Chegeni katika semina hiyo.
Swali hilo halikutegemewa na Dk Hosea na lilionekana kumuudhi na kulazimika kuchukua kipaza sauti na kusitisha maswali na kuanza kujibu kwa ghadhabu.
“Hapa siyo jukwaani hivyo tusilete siasa. Nipo hapa kwa ajili ya kufundisha na kama ni suala la Richmond waziri mkuu alishaliongelea na ndiyo mwenye dhamana ya kujibu hilo. Mimi sina jibu kwa hilo na kama mtu hapendi kuvuliwa nguo kwanini umvue mwenzako,” alisema Dk Hosea.
“Mjadala huu aachiwe Waziri Mkuu Mizengo Pinda na aliyeuliza swali hilo hanitendei haki kwani hakuna hoja nyingine ya maendeleo kwa jamii ambalo inaweza kujadiliwa… mbona mnang’ang’ania kujibu hilo pekee.
“Najua kuna watu wanatumiwa ili niongee halafu nibabaike katika kujibu na nishindwe kufanya kazi yangu. Mbona mnang’ang’ania jambo hilo tu wakati kuna hoja nyingine za maendeleo kwa jamii. Kuhusu suala la Richmond sijibu ng’o.”

5 Comments »

  • Anonymous said:

    Mhariri

    Mimi binafsi huwa ni shabiki wa Bwana Mjengwa kulingana na mtazamo wake wa kijamii. Niliposikia kuwa wameshirikiana kuanzisha gazeti nilifikiri mbadala wa iliyokuwa RAI yetu Watanzania umepatikana. Lakini kwa uandishi huu, na ushabiki huu!!!! nashawishika kujiuliza mara mbili mbili.

    Wasalaam.

  • Awinia said:

    Hapa tumeliona tatizo…kazi ni tiba tuache kuripoti tuuuuu; kilichotakiwa hapo ni Kuanza na Wakurugenzi waliolipa hizo posho na kumalizia na Bwana Slaa na wenzake kurudisha posho hizo na adhabu kama vifungu vinavyosema..kinachotuua siku zote ni matabaka kama haya kibaka anapata suluba hawa wanachukuliwa kuwa ni bahati mbaya…..

  • Kitoto said:

    “Katika ukaguzi tulioufanya tuliweza kubaini matumizi yasiyostahili yenye thamani ya Sh 8,472,200 ambayo yasingeweza stahili kulipwa kwa kutumia fedha za miradi ya TASAF,” anasema CAG kupitia ripoti yake ya ukaguzi kwa mwaka ulioshia Juni 30, mwaka 2008, ripoti ambayo hata hivyo imekwishawasilishwa bungeni.
    Maelezo yaliyotolewa kwa CAG kuhusu malipo hayo yanasema; “Posho kwa ajili ya vikao vya kamati ya Bunge ya hesabu za serikali za mitaa Agosti 7 hadi 16 mwaka 2007 yalikuwa Sh 1,050,000.
    Kutokana na kubainika kwa hali hiyo huenda hadhi ya wajumbe wa kamati hiyo inayoongozwa na Dk. Wilbroad Slaa, Mbunge wa Karatu, ikaingia doa mbele ya umma wa Watanzania

    Nimenakiri kipande hicho toka katika habari kuu kuonesha ushabiki wa mwandishi na nia yake ya kutaka kuchafua Dr slaa. kwa mara ya kwanza niliona habari hii kwenye website fulani( sitaisema hapa)na mmoja wa wachangiaji pale alitoa ufafanuzi ambao mimi pia nilikuwa naufahamu. Ni kuwa kipindi kilichotajwa na CAG kuwa kamati hii ilikula posho mara mbili, kamati hii ilikuwa chini ya Mh. Mghana Msindai na siyo Dr Slaa kama muandishi alivyotaka jamii ilewe, japo ni kweli kuwa kamai hiyo sasa inaongozwa na Slaa, mwandishi hakuwa na sababu ya maana kuweka kichwa cha habari kama alichotumia. Kwa mtu yeyote mwenye kujua vyema kuhusu hili hato sita kusema na kuamin kuwa mwandishi ama kwa makusudi au kwa kutokujua ametoa habari iliyolenga kumchafua Slaa. kama alikuwa anahaja ya kuvutia wasomaji (maana jina la Dr Slaa siku hizi ni biashara nzuri tu kwa waandishi) kwa heading ile basi mahali fulani ndani ya habari yake angetoa ufafanuzi huu kuwa japo kamati ile ilikula posho mara mbili mwaka 2007 ilikuwa haongozi na Slaa!
    Mimi nadhani mwandishi anatakiwa kutoa ufafanuzi katika toleo lijalo,la naogopa kusema Kwanza jamii litapoteza mvuto kwa wasomaji muda si mrefu, kwani litaonekana kama linatumiwa na kikundi fulani kwa maslahi ya watu fulani.

  • Anonymous said:

    Maggid Unatumika?

  • amani said:

    Kwa upande wangu nadhani si suala la kutumika au kutotumika. Kama ni kweli kamati hiyo ilikuwa haiongozwi na Dr. Slaa wakati huo basi ni wazi mwandishi alipaswa kutoa ufafanuzi ndani ya habari hii. Hata hivyo msitake kutaka mie na Watanzania wenzangu waamini kuwa DR. Slaa ni mtu MTAKATIFU ambaye katu kwa namna yeyote hawezi kutuhumiwa/kukumbwa na kashfa na pengine kutiwa hatiani. Mtu ataendelea kuwa hana hatia yoyote hadi hapo mamlaka husika itakapothibitisha vinginevyo. Sote tunaona jinsi CHADEMA wanavyovihujumu vyama vingine vya upinzani kwa kutangaza kuwa wao wnaungwamkono wakati hakuna vikao rasmi vilivyokaa kufanya maamuzi hayo ya pamoja. NATAMBUA MCHANGO MKUBWA ALIOUTOA DR. SLAA WA KUPIGA VITA ULAJI RUSHWA NA UFISADI lakini ninachotambua na kukijua mimi ni kuwa pamoja na wish yake ya kusaidia nchi, Mwansiasa yeyote anatajia kuona ujira wa haya anayoyasema ni UMAARUFU na KUUNGWA MKONO YEYE PAMOJA NA CHAMA CHAKE. Hivyo iwapo watu watajengewa kumwamini mwanasiasa fulani kuna hatari ya kulaghaiwa kwa sababu ya USHABIKI. Slaa ni kada wa CCM toka akiwa Chuo Kikuu Rome, na alihama CCM baada ya kunyyimwa madaraka aliyokuwa anayawania. Sina maana ya kupuuza mchango mkubwa na huruma ya DR.

Weka maoni yako hapa!

Add your comment below, or trackback from your own site. You can also subscribe to these comments via RSS.

Be nice. Keep it clean. Stay on topic. No spam.

You can use these tags:
<a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <strike> <strong>

This is a Gravatar-enabled weblog. To get your own globally-recognized-avatar, please register at Gravatar.