Home » Featured, Habari, Headline

Gari La Kigogo Chadema Anayekwepa Kodi Ladakwa

7 October 2011 517 views One Comment

Gari lenye namba T 637 ADA aina ya Toyota Land Cruiser, la Coleman Mushi, linalodaiwa kukwepa kulipa kodi tangu Juni 2010, likiwa kituo cha polisi makao makuu Dar es Salaam jana (Ijumaa) mchana kabla ya kurejeshwa kwa mmiliki wake jioni. (PICHA NA MPIGA PICHA WETU)

Na Mwandishi Wetu
GARI la kigogo mmoja anayefanya kazi Mamlaka ya Bandari Tanzania (THA), Coleman Mushi, linalodaiwa kukwepa kulipa kodi, limetiwa mbaroni na polisi.

Habari zilizonaswa zimebainisha kuwa kigogo huyo ambaye ni mfuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), alikamatwa maeneo ya Salender Bridge juzi (Alhamisi) usiku.

Gari hilo lilikamatwa kutokana na mtego wa polisi wa usalama barabarani kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) waliodokezwa hila la kigogo huyo kwa barua ambayo nakala yake ilipelekwa kwa Kamishna Mkuu wa TRA, Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga na Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) Said Mwema.

Kwa mujibu wa barua ya Oktoba 4 mwaka huu, iliyoandikwa na mkazi wa Dar es Salaam, George Joseph kwenda kwa Kamishna Upelelezi wa Kodi – TRA, gari hilo lenye namba T 637 ADA aina ya Toyota Land Cruiser, linadaiwa kukwepa kulipiwa kodi tangu Juni 2010.

Barua hiyo ilieleza kuwa mmiliki wake hajawahi kulipa kodi ya leseni ya kuliruhusu kutembea barabarani na amekuwa akiliendesha kila siku huku kutoka Gongo la Mboto anapoishi kwenda maeneo mbalimbali Dar es Salaam, akidai yeye ni Ofisa wa Usalama wa Taifa.

Kwa mantiki hiyo, amekuwa akiikosesha mapato Serikali kwa vile gari hilo licha ya kutokuwa na kibali cha kutembea barabarani, pia halina bima na hata mmiliki hana leseni ya kuendesha gari.

Mtego uliowekwa juzi ulimnasa Mushi akiwa Salender Bridge ambako pia yeye ni kiongozi wa klabu hiyo, na gari hilo kupelekwa makao makuu ya polisi.

Habari zimedokeza kuwa uongozi wa TRA uliwaagiza polisi walikabidhi gari hilo kwa mamlaka hiyo baada ya kumaliza ukaguzi wao, lakini jana (Ijumaa) jioni, ilidokezwa kuwa mmiliki wa gari hilo alikabidhiwa kwa agizo la Msaidizi wa Kamanda wa Usalama Barabarani.

Mpasha habari alidokeza kuwa kamanda msaidizi huyo wa polisi wa usalama barabarani alijitetea kwamba aliliachia gari hilo baada ya mmiliki kulipa faini TRA, huku akidai kwamba barua ya mamlaka hiyo hakuipata.

Kamishna Upelelezi wa TRA ambaye hakupenda jina lake litajwe alidai hakuridhishwa na kitendo cha polisi kuliachia gari hilo, na hata Msaidizi wa Kamanda wa Usalama Barabarani alipopigiwa simu selula yake, iliita bila kupokelewa. Juhudi za kumtafuta Kamanda Mpinga bado zinaendelea ili atoe ufafanuzi kinagaubaga kuhusu kuachiwa kwa gari hilo.

One Comment »

  • Elliptical said:

    This is the exact info i’m looking for, thanks! Arron