Mrisho Mpoto: Watanzania Tunakufa Kwa Roho Chafu!
JUZI hapa nilipata bahati ya kusafiri na Mrisho Mpoto. Safari yetu ilianzia Iringa kwenda Njombe. Tulikuwa na saa tatu pamoja kujadili masuala juu ya jamii yetu.

Mpoto ni mmoja wa wasanii mahiri na maarufu sana nchini kwa sasa. Na kwangu mimi, Mpoto ni mwanafalsafa anayeifikia jamii pana kwa tungo zake zenye kufikirisha.

Tulipofika eneo la Nyororo, Mufindi, Mpoto alishuka kwenye gari ili tununue chupa ya maji ya kunywa. Ndani ya dakika tatu tukawa tumezungukwa na watu wasiopungua 50. Wote walitaka kumwona Mpoto na kuzungumza naye. Sauti za ’ Mjomba, Mjomba!” zilisikika zikiita.

Tuliondoka mahali hapo baada ya yeye kupiga picha ya pamoja na mashabiki wake. Baadaye alinitamkia; ” Hawa ndio watu wangu, leo wananikubali kwa kuwa nawasemea. Siku nikiacha kuwasemea, watapatwa na huzuni. Watanikataa, nami sitakuwa mtu mwenye furaha pia”. Hapo tukajikita katika kujadili maana ya msanii au mwandishi kuwa kioo cha jamii.

Baadaye kwenye mazungumzo yetu niligusia kauli ya Mpoto kwenye moja ya matangazo ya kijamii redioni. Kwenye tangazo hilo anatamka; ” Kwenda huko, utakufa kwa roho yako mbaya!”.

Nilimwuliza Mpoto swali la kifalsafa; ”Je, binadamu tunakufa kwa roho mbaya au roho chafu?”

”Kaka Maggid, naiona mantiki ya swali lako. Kama nitakunjua viganja vyangu na kuitema roho yangu kisha nikaiangalia… lakini fafanua kwanza fikra zako,” alijibu Mpoto.

Nikafafanua, kuwa binadamu hatukuumbwa kuwa wengine wana roho mbaya na wengine nzuri. Sote tumeumbwa na roho nzuri isipokuwa mazingira ndiyo yanayotufanya wengine tukawa na roho chafu na wengine roho safi. Ndiyo, roho nzuri tulizoumbwa nazo zinachafuka. Tunakuwa ni binadamu wenye roho chafu. Na hakika, Watanzania wengi tunakufa kutokana na roho chafu, zetu wenyewe au za wenzetu.

”Mh!” Anaguna Mpoto. Ananiacha niendelee.

Maana, ni mtu mwenye roho chafu tu anayeweza kuhujumu mradi wa kuangamiza malaria inayosababisha vifo vya maelfu ya watoto na watu wazima kwa tamaa zake binafsi. Ndiyo, kuhujumu mradi wa kuzuia malaria ili apate fedha za kufanya mambo ya fahari au hata kununua uongozi wa kisiasa. Kwa mwanadamu, ni heri ufe kwa kupambana na anayehujumu mradi wa kuangamiza malaria kuliko kufa kwa malaria inayotokana na mbu anayesababisha malaria.”

Tukazidi kuzama kwenye la fikra. ”E bwana, Makambako hapa. Nafurahi kila ninapokuwa mbali na Dar es Salaam,” anatamka Mpoto.

”Kwanini unafurahi kuwa mbali na Dar?” Namwuliza Mpoto.

”Maggid, angalia nje. Hawa ndio Watanzania wanaopambana kila kukicha kwa maendeleo ya nchi yetu na kuna wachache mijini wanaodhani kuwa ni haki yao Watanzania hawa kuishi katika hali ya ufukara pamoja na rasilimali zote hizi tulizonazo.”

Kwa hiyo ndio maana umefurahi kuwa mbali na Dar?”

”Wakati mwingine ni muhimu kutoka nje ya miji mikubwa kama Dar, kwenda mbali na kuona hali halisi,” ananijibu Mpoto.

Turudi kwenye mada ya Watanzania na roho zetu chafu. Na hili lina mantiki katika kipindi hiki cha kampeni za Uchaguzi Mkuu. Nilimsimulia Mpoto kisa nilichopata kukisimulia huko nyuma. Kisa cha bwana aliyemwomba sana Mungu amsaidie. Siku moja akaambiwa; sala zako zimekwishakusikilizwa, isipokuwa, Mungu atakusaidia kwa sharti moja; kwamba kile atakachokupa wewe, basi, jirani yako atampa mara mbili yake.

Bwana yule akahitaji muda wa kwenda kutafakari kabla hajampa Mungu jibu. Akarudi na jibu; ” E Mola wangu, naomba unipe chongo, utoboe jicho langu moja. Bwana yule alikuwa tayari awe na chongo ili jirani yake awe kipofu kabisa!

Na hakika, Watanzania wa kawaida walio wengi si watu wenye roho chafu. Isipokuwa, tuna bahati mbaya ya kuwa na baadhi ya viongozi wabinafsi na wenye roho chafu huku wakilindwa na mapungufu ya kimfumo katika matendo yao maovu.

Ni viongozi ambao, kama kuna kuchagua kati ya wao kupata kimoja na wanaowaongoza kupata viwili, basi, wana hiari ya kuchagua kupata kilema cha mguu mmoja ili wanaowaongoza wawe viwete.

Ndani ya roho ya mgombea hana chema anachowatakia wapiga kura wake. Anajiangalia yeye tu. Yote hii inatokana na kukithiri kwa ubinafsi. Na mapungufu ya kimfumo nayo yanawasaidia viongozi hawa wabinafsi kutenda maovu yao kwa wananchi bila hofu. Katika kuendekeza ubinafsi wao, unaweza kabisa kuamini, kuwa viongozi hawa wanawachukia Watanzania wenzao.

Ni kwa sababu ya ubinafsi na roho zao chafu. Na anachoshindwa kuelewa kiongozi huyu anayechukia maendeleo ya mpiga kura wake ni ukweli kuwa maendeleo ya mtu huyo binafsi yatakuja kwa namna moja au nyingine kumnufaisha hata yeye na Taifa kwa ujumla. Na tuna wabunge wengi watakaoangushwa na wapiga kura wao katika uchaguzi wa Oktoba kwa sababu wameshindwa hata kuficha makucha yao ya ubinafsi.

Kwa wabunge hawa, miaka mitano ya kukaa bungeni imewaletea neema kubwa wao binafsi huku majimbo yao bado yakiwa nyuma sana kimaendeleo. Lakini, kuna wabunge ambao, wamejitahidi sana. Na mifano ya juhudi zao za kuwaletea maendeleo watu wa majimbo yao inaonekana.

Hawa watatendewa haki, maana, wananchi wa majimbo husika wanawajua na wanajua waliyoyafanya kwa maendeleo ya majimbo yao. Hakika, wananchi wamechoka kuvutwa nyuma kimaendeleo. Kuvutwa nyuma kunakosababishwa na baadhi ya viongozi waliowapa dhamana za uongozi.

Mathalan, katika nchi hii hutokea anayehusika na kuwasaidia Watanzania wenzake kupata nafasi za kwenda kusoma nje ya nchi akatoa nafasi hizo kwa upendeleo. Ataanza na familia yake, ndugu na atamalizia na jamaa na rafiki zake. Wakisha hao yuko tayari nafasi hizo zibaki tupu kuliko kuwasaidia Watanzania wengine.

Kuna vyuo vya humu duniani utakuta wamejaa Waafrika kutoka nchi nyingine, iwe Ghana, Nigeria, Kenya na kwingineko. Lakini utashangaa ni kwa nini idadi ya Watanzania ni ndogo sana au hawako kabisa kwenye vyuo hivyo. Tofauti hapa ni ukweli kuwa wenzetu katika mataifa mengine wanasaidiana sana katika kupashana taarifa juu ya kuwapo kwa vyuo hivi na namna ya kupata nafasi hizo. Mathalan, nchi kama Ghana ikitengewa nafasi 50 kwa mwaka katika vyuo vya nchi ya kigeni, basi idara husika katika Ghana itahakikisha nafasi hizi zinajazwa.

Tuna haja ya kufanya jambo moja muhimu kwa sasa; tujenge moyo wa uzalendo na utaifa. Tuipende nchi yetu. Tupendane kama Watanzania. Ubinafsi uliokithiri na kuwa na roho chafu, hususan, kwa baadhi ya tuliowapa dhamana za uongozi unatuweka mahala pabaya kama Taifa. Huko tunakokwenda tatizo hili litatutafuna. Ndiyo, roho zetu chafu zitasababisha Taifa kuangamia. Mtaona ishara…

Simu:

0754 678 252

Barua-pepe:

mjengwamaggid@gmail.com

Blogu:

mjengwa.blogspot.com

Hotuba Yangu Kwenye Uzinduzi Wa Kwanza Jamii, Njombe
” Njombe Mpooo?”x2

Jibu: ” Tupoo!” x2

Ndugu Mgeni wa Heshima,

Ndugu Wageni waalikwa,

Mabibi na Mabwana.

Nina furaha kubwa kupata bahati ya kushiriki tukio hili kubwa la uzinduzi wa jarida la Kwanza Jamii hapa Njombe. Nasema hivyo kwa vile ingawa mimi ni mwalimu kitaaluma, nami nimekuwa mwandishi wa makala za uchambuzi kwa miaka 20 sasa.

Kusanyiko hili linanishawishi nisimulie kisa kifupi chenye  mantiki kwa  kinachofanyika hapa hii leo. Maana, kila mmoja wetu amekuja hapa kuona na kusikiliza akiamini kuwa kuna atakachojifunza. Ndio, inahusu maarifa.

Zamani sana katika Ugiriki ya Kale alipata kutokea mwanafalsafa aliyeitwa Socrates. Bwana huyu siku moja alionekana mchana wa jua kali akitembea sokoni huku akimulika kurunzi yake ( tochi). Watu pale sokoni walimshangaa sana Socrates. Kuna waliomwendea karibu na kumwuliza; ” Socrates, kulikoni leo unatembea mchana wa jua kali huku ukimulika tochi?”

Socrates akawajibu; ” Kwenye nuru hii, kuna walio gizani!” Lile lilikuwa tendo la kifalsafa lililoakisi hali halisi aliyoiona Socrates katika jamii iliyomzunguka; kwamba bado kulikuwa na wanajamii waliojifunika vilemba vya ujinga. Hata mchana kwao ilikuwa ni giza.

Ndio, inahusu maarifa. Na Socrates yule anatwambia kuwa kuna milango mitatu ya ufahamu ambamo mwanadamu anaweza kuifungua ili kupata maarifa. Hakuna maarifa yatokanayo nje ya milango hiyo mitatu. Mlango wa kwanza ni maarifa yatokanayo na uzoefu, Wagiriki wanaita Fronesis. Bibi yangu mimi aliweza kuangalia juu mawinguni na kutamka kuwa mvua itanyesha. Hakusoma hata darasa moja. Alikuwa na maarifa yalitokana na uzoefu wake.

Mlango wa pili wa maarifa ni yale yatokanayo na elimu tunayoipata shuleni, Wagriki wanaita Episteme. Niwaulize nyie wanafunzi mnaonisikiliza; kumi ukitoa moja inabaki ngapi?

(” Tisa!” )Kama jibu ni tisa nikiwauliza kuwa kwenye mti kuna ndege kumi na mimi nimerusha jiwe nikampiga mmoja watabaki wangapi?

” Sufuri! Hakuna!……)

Sasa basi, tunaelewa kuwa jibu la kumi kutoa moja litatokana na mazingira ya swali lilipoulizwa, maana katika swali hilo mtoto wangu wa miaka tisa alinijibu atabaki ndege mmoja kama jiwe limempata na kuanguka chini! ( Kicheko) Ndio, hapa tunaona umuhimu wa kuchanganya elimu ya darasani na uzoefu wetu.

Mlango wa tatu wa maarifa ni yale yatokanayo na kipaji, Wagiriki wanaita ‘ tekne’. Hata neno teknolojia linatokana na neno hilo la Kigiriki. Kwamba baadhi yetu hapa, kama wazazi, tumeua vipaji vya watoto wetu kwa kuwakatisha tamaa tangu utotoni. Leo mtoto wako anaimbaimba, unamwambia ‘ acha kupiga kelele!’. Huwezi kujua, labda angekua akawa kama Mrisho Mpoto. Na nyie wanafunzi hapa mnapokuwa shuleni wakati mwingine mnaua vipaji vya wenzenu kwa kuwakatisha tamaa.

Ndugu zangu,

Na ili tufanikiwe katika tuyafanyayo. Tujikwamue na kupiga hatua za maendeleo, kwa mtu mmoja mmoja, kikundi cha watu au taifa, ni sharti tuzingatie  ‘ K’ tatu; nazo ni Kujitambua, Kujiamini na Kuthubutu.  Maana kama walivyotuimbia  wale vijana wasanii wa mziki wa kizazi kipya wa  ‘ Njombe Runners’; Kwamba kujikwamua si suala la taasisi pekee, Si suala la serikali pekee.

Hivyo basi, tuanze SASA  kujenga uwezo wa Kujitambua. Tuanze SASA kujenga moyo wa Kujiamini. Tuanze SASA kujenga moyo wa Kuthubutu.

Ndio, Tunaweza kuyafanya hayo. Yes, We Can!

Ahsanteni Sana Kwa Kunisikiliza.

Hawa Ndio Mashujaa Waliolifikisha KwanzaJamii Kwa Wanajamii Wa Njombe!
Nduguzanguni,

Bila shaka baadhi yenu mmefikiwa na habari za jarida la ‘Kwanza Jamii’ kurudi tena kwa wanajamii wa Njombe.

Nachukua fursa hii kuwashukuru wote waliojitolea kuchangia kazi zao za kiuandishi katika jarida la Kwanza Jamii tangu lilipotoka kwa mara ya kwanza. Mchango wao ndio uliopelekea Kwanza Jamii kufahamika kwa haraka na kupendwa na wasomaji. Na hata baada ya Kwanza Jamii kushindwa kuendelea kutoka mitaani kutokana na kukosa uwezo wa kulipia gharama za uendeshaji kulikotokana kwa kiasi kikubwa na kukosekana kwa watangazaji gazetini, bado Kwanza Jamii limekuwa likiuliziwa na wasomaji wake kutokana na mchango wenu. Na ndio imepelekea pia Jumuiya ya Daraja kutaka kuunga mkono juhudi za Kwanza Jamii katika kuifikia jamii . Na hapa sitasahau mchango mkubwa kabisa wa wafuatao; Bi. Subi Sabato, Bi. Naima Besta, Profesa Joseph Mbele, Born Again Pagan, Joseph Mihangwa,Profesa Bwenge, Padri Privatus Karugendo, Freddy Macha, Eliamani Laltaika, Jeff Msangi, Dr. Masanzu Matondo, Mohamed Ang’olwa, Mheshimiwa Pius Msekwa, Mohammed Seif, Kamala Lutasinsibwa, Mussa Ngarango ( Mchora Katuni) na Beka ( Graphic designer), Bilal ( Masoko na Usambazaji) na bila kuisahau familia yangu. Ambao sijawataja, sijawasahau na jamii haitawasahau kwa kujitolea kwenu. Mbarikiwe Sana.

Maggid

Iringa,

Septemba 2, 2010.

( Pichani ni Ofisi za Kwanza Jamii, Kinondoni Biafra. Ndio ofisi iliyotumika kwa shughuli za Kwanza Jamii tangu toleo la kwanza hadi tuliposimama kuchapa.)

Kwanza Jamii Limerudi Kwa WanaJamii Njombe!
Hatimaye Jarida la Kwanza Jamii limerudi kwa wanajamii. Hii inatokana na Jumuiya isiyo ya Kiserikali ya Daraja yenye makao yake Mkoa mpya wa Njombe kuchukua jukumu la kugharamia uendeshaji wa jarida hilo na kuwa kiungo kati ya wanajamii na halmashauri ya wilaya Njombe. Hii ina maana , kuwa jumuiya ya daraja kwa ufadhili kutoka Uingereza wa muda wa miaka mitatu kwa mkataba wa mwaka mmoja mmoja. Daraja itagharamia gharama za uchapaji, wahariri, waandishi na kusimamia usambazaji huku umiliki wa jarida hilo ukibaki katika kampuni ya Ikolo Investiment iliyokuwa ikitoa gazeti hilo hapo awali. Kwanza Jamii linakuwa gazeti la Kwanza la Kijamii mkoani Njombe na pengine katika Kanda ya Nyanda Za Juu Kusini. Pichani juu ni Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Mama Sarah Dumba akitoa hotuba ya uzinduzi wa Jarida la Kwanza Jamii Njombe kwenye viwanja vya Sabasaba Agosti 30, 2010. Kwa kuanzia, Kwanza Jamii litakuwa likitoka mara moja kwa mwezi na baadae litatoka kila wiki. Litaanza kwanza na habari za Njombe na kama litapata mafanikio litasambaa katika wilaya nyingine za mkoa huo.  Nachukua fursa hii kuwashukuru wote waliojitolea kuchangia kazi zao katika jarida la Kwanza Jamii tangu lilipotoka kwa mara ya kwanza. Mchango wao ndio uliopelekea Kwanza Jamii kufahamika kwa haraka  na kupendwa na wasomaji. Na hata baada ya Kwanza Jamii kushindwa kuendelea kutoka mitaani kutokana na kukosa uwezo wa kulipia gharama za uendeshaji kulikotokana kwa kiasi kikubwa na kukosekana kwa watangazaji gazetini, bado Kwanza Jamii limekuwa likiuliziwa na wasomaji wake kutokana na mchango wenu. Na ndio imepelekea pia Jumuiya ya Daraja kutaka kuunga mkono juhudi za Kwanza Jamii  katika kuifikia jamii . Na hapa sitasahau mchango mkubwa kabisa wa wafuatao; Bi. Subi Sabato, Bi. Naima Besta, Profesa Joseph Mbele, Born Again Pagan, Joseph Mihangwa, Padri Privatus Karugendo, Freddy Macha, Eliaman Laltaika, Jeff Msangi, Dr. Masanzu Matondo, Mohamed Ang’olwa, Mheshimiwa Pius Msekwa, Kamala Lutasinsibwa, Mussa Ngarango ( Mchora Katuni) na Beka ( Graphic designer), Bilal ( Masoko na Usambazaji). Ambao sijawataja, sijawasahau na jamii haitawasahau kwa kujitolea kwenu. Mbarikiwe.

Maggid

Iringa,

Septemba 2, 2010.

Mrisho Mpoto Nyumbani Kwa ‘ Mwenyekiti’
Ijumaa ya juma la jana nilimkaribisha mdogo wangu Mrisho Mpoto nyumbani ninakoishi hapa Iringa. Mrisho na mimi tulikuwa na safari moja ya kwenda Njombe. Safari iliyoanzia nyumbani kwangu. Akiwa kwangu alinikuta sijafunga vya kwenda navyo. Wakati Mrisho na msanii mwenzake Ismael wakipata chai na juice mwanangu aliwatumbuiza kwa ‘gitaa la solo’ huku mie nikipiga pasi moja ya mashati yangu ya batiki. ( Kulia pichani). Ni mashati yale yale msionisha kunisema nayo!

Baada ya kutoka nyumbani nilimwandalia Mrisho ziara ya miguu kwenye mitaa ya kati ya mji wetu wa Iringa. Ziara ikaishia studio za Ebony FM alipofanyiwa mahojiano. Kisha akawatengenezea ‘jingles’ za vipindi vyao vya redio. Baada ya hapo tukaingia kwenye ‘ Bi Mkora’ wangu na kuanza safari ya kwenda Njombe. Nina ya kusimulia zaidi ya njiani, na picha pia.

Waumini Wamlalamikia Askofu Jimbo La Rulenge
Asante mwenyekiti kwa kazi nzuri uifanyayo hasa kutuelimisha kwa njia ya Blog, nasema hongera sana mkuu! Hivi karibuni nilikuwa ngara mkoani kagera kufanya utafiti kwenye masuala yangu ya shule, lakini nilikutana na malalamiko pamoja na simanzi za wakazi wa Rulenge-ngara ambao wanadai kuwa Askofu wao amehamisha makao makuu ya jimbo kutoka rulenge kwenda ngara mjini bila ridhaa ya waumini/wananchi!! is this democracy??

Mdau: Pastory Paul

Bi Mkora: Kinachochangia Mwenzako Asijishughulishe Kitandani
Pole mdau kwa yanayokukuta,

Kuna vitu vingi vinaweza kuchangia hayo kama walivyokueleza wadau waliotangulia kutokana na uzoefu wao ambao nitawaita masomo. Kungwi Bi Mkora ana

1. Mko kwenye uhusiano wa namna gani? Mke na mume, au bibi na bwana au wa kirafiki? Aina ya uhusiano mlionao mara nyingi huchangia katika namna ambavyo mwanamke atashiriki katika tendo la ndoa. Ikiwa yuko kwenye mahusiano yasio na uhakika wala mwelekeo basi mara nyingi hushiriki kwa hofu na wasi wasi wa kupata mimba nje ya ndoa, na kuogopa kuwa atakapopata hiyo mimba anaweza kuachwa solemba na mtoto wake. Pia anaweza kuwa na hofu ya kukutwa na mwenye mali maana yake sie wanawake huwa hatuamini kuwa mwanaume anaweza kukaa siku zote hizo hana mwenyewe, kwa hiyo wakati mwenzio anajishughulisha wewe kichwa chako kinazunguka kuhusu kufumwa na mwenyewe, au kupata mimba zisizo na matarajio. Hali hii ya kutojiamini inaweza kuondoshwa pale tu ambapo mwanamke atakuwa yuko kwenye mahusiano yaliyo thabiti na ambayo ana uhakika kuwa “wote ni waongo mwenyewe ni yeye”.

Hilo moja pili inawezekana mazingira mnayofanyia hiyo shughuli hayana faragha ya kutosha, hili nalo mara nyingi ni kikwazo, kuna wanawake ambao wanapenda sehemu yenye faragha sana, na hawapendi watu wengine wajue kuwa sasa hivi alikuwa kwenye shughuli maalum. Je kwenye hiyo nyumba unaishi na watu wengine? Kwa mfano labda wewe ni mwanafunzi na unashea nyumba na wanafunzi wenzio hata kama ni watu wazima na yeye anaona kuwa akitoka nje asubuhi, au muda wowote ule basi wenzio mnaoshea nao nyumba wanaweza kumuona huyoo, bibie keshashughulikiwa sasa. Hata kama ni mke wa ndoa halali yako kabisa lakini uhalisia kundi kubwa la wanawake wanapenda faragha. Na nyumba zenyewe za uzunguni za makaratasi/mabox, anaogopa kuwa sauti inaweza ikatoka nje ikawafikia wenzio, au anaogopa kitanda kitapiga kelele. Amini usiamini hiyo ni sababu kubwa. Kama ni hivyo jaribu kutafuta faragha halafu uone itakuwaje.

Tatu kama yote hapo juu sio, ni mkeo, mnaishi kwenye mahali ambako kuna faragha ya kutosha, inawezekana mwenzio amejawa na simanzi au sononi. Pengine ana depression kutokana na maisha tu jinsi yalivyo au pengine kutokana na jinsi ulivyombadilikia, je umewahi hata mara moja zaidi ya shughuli ya kitandani, kumfurahisha, kumchekesha, kumnunulia zawadi, kumsifia na kumfanya asijione mpweke huko mliko? Maana kuna wanaume wengine hasa wa Kitanzania yaani wao pamoja na kuwa ughaibuni utakuta mkewe anamuacha nyumbani, kazi yake ni shughuli za nyumbani, kulea watoto, na kufanya kazi ya kuingiza kipato, hata siku moja hawezi kusema leo (kama wana watoto) tumwite babysiter mie na wewe tutoke japo twende sinema, au park tu tukakae wawili tutazamane macho! Kaka zangu, wadogo zangu, acheni tabia ya uselfish kwa wake zenu, mpeleke japo akale ice cream mjini sio tu ndio umempata maid wa kukufanyia shughuli zako. Na siku moja moja agiza take away, au ingia jikoni msaidie sio lazima upike lakini msaidie kuandaa chakula, kufanya usafi ili kumpunguzia mwenzio mzigo wa kazi. Kazi za ndani zinachosha, na ukizingatia kama anafanya kazi nyingine au anasoma na yeye, usiku ukifika yuko hoi bin taabani, halafu tena mume anakuja na yeye anataka mbio za marathoni kwanini asigeuke upande wa pili? Kachoka ati, shughuli juu ya shughuli!

Mwisho kabisa inawezekana mwenzio ni hanithi, yaani hapati hisia zozote kwenye suala zima la kufanya tendo la ndoa hata ukifanyaje yeye anaojionea bora liende. Hapo dawa ni kuonana na madaktari ambao wanaweza kumpa dawa za kumsaidia. Ndio eeh mnashangaa nini kama vile ambavyo wako mahanithi wanaume na wanawake pia kuna mahanithi ambao hawapati hisia zozote na tiba yake inapatikana mahospitalini na kutumia diet ambazo tuliwahi kuzungumzia siku za nyuma, mambo ya supu ya pweza, na ngisi na nini!

Wenu Bi Mkora!

Mdau Ubelgiji: ” Mjengwa, Ngoja Nikukosoe!”
Habari yako mjengwa.

Nachukua nafasi hii kukupongeza,kwa kutupatia habari za mara kwa mara, lakini Mjengwa ngoja nikukosoe mambo fulani fulani,mfano kuweka picha bila maelezo?,ni kweli kua ujumbe unatakiwa kutolewa kwa picha ,lakini ktk Blog kama hii,huna haja ya kuweka picha bila maelezo.

La pili ni kukuhusu wewe,mwenyewe,sio lazima kutoa taarifa kua hapa nipo msamvu,mara nipo Mikese,wewe andika habari za Mikese watu tutaelewa tu mzee

La tatu ni kua,kuna sababu gani ya kuweka picha na kusema kua Msamvu leo mchana,mara Mbuyuni jana jioni,so what?! Try to improve!!

Kaka mimi si ku-challange ila tafsiri,inakua kama vile unazurura,ila ukitueleza jinsi ndizi zilivyo hapo Mikese,au picha za magunia ya mchelle kule mwanjelewa,hapo sawa hata sisi tuliopo huku nje tunajua kinachoendelea huko Home.

Nakutakia kazi njema yenye mabadiliko!

Kenny

Antiwerp-Belgium!

Swali Kwa Bi Mkora: ” Mwenzangu Hajishughulishi Kitandani, Nifanyeje?”
NAFURAHI SANA WAJUMBE WATOAVYO MAWAZO HUSUSANI YA KUWEKA NDOA YENYE FURAHA NA UPENDO.

SUALA SI KUMWANDAA MWANAMKE PEKEE ILA KUANDAANA WOTE KABLA YA KUFANYA MAPENZI.

KWA UPANDE WANGU NAOMBA NISAIDIENI:

NIKIKIWA NAMWANDAA MKE WANGU HUSUSANI KWA KUCHEZA CHEZA KITANDANI, KUSHIKANA SHIKANA UTAKUTA MKE WANGU YUPO KIMYA TU NA YEYE HAJISHUGHULISHI KWA CHOCHOTE KABISA, WALA NAYE KUKUCHEZEA CHEZEA AU HATA KUKUSHIKA UUME. MPAKA NAWEZA NIKANANIHII , YEYE YUPO KIMYA.HATA LUGHA YA KIMAHABA HANA.SIJUI NIFANYAJE.

Mdau Emmanuel, USA.

PS: Wengine mnakaribishwa kuchangia uzoefu wenu katika maswali haya ya kimahusiano ambayo ni moja ya sehemu muhimu katika maisha ya kijamii. Muhimu ni staha katika uchangiaji huo. Mhariri.

Kuwahukumu Maharamia Wa Kisomali Isiwe Jukumu La Nchi Za Pwani Ya Bahari Ya Hindi Tu
NA MWANDISHI MAALUM

NEW YORK-Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa  limetakiwa kutoziachia  mzigo mzito  nchi ambazo zimejitolea utekeleza kwa niaba ya jumuia ya Kimataifa, jukumu la  kuwapokea,  kuwahukumu na kuwafunga maharamia na majangili ya kisomali yanayoendesha uhalifu wao katika pwani ya Somalia na maeneo mengine.

Uhauri huo   ambao umeungwa mkono na mataifa mengi, umetolewa na mwakilishi wa serikali ya Uingereza katika Umoja wa Mataifa, Bw. Mark Lyall Grant. Wakati wa mkutano wa Baraza Kuu la Usalama uliokuwa ukijadili  ripoti na mapendekezo yaliyotolewa na Katibu   Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban ki Moon, kuhusu namna gani jumuia ya kimataifa itakavyoweza kuboresha na kuongeza kasi ya kuwafikisha mbele ya mkono wa sheria  maharamia  wa kisomali.

“ Kazi ya kuwahukumu, kuwafunga na kuwahifadhi  maharamia  na  majangili wa kisomali, ni kazi kubwa na  nzigo, ni mzigo ambao nchi hizo hazitakiwa kuubeba peke yake, Baraza  Kuu la Usalama na Jumuia  ya Kimtaifa tunapaswa kuwasaidia ni jukumu  letu sote” akasema balozi huyo.

Akasema kuwa hadi sasa Mashirika ya  Umoja wa Mataifa  yanayoshughulikia  dawa za kurevya na  uhalifu (UNODC) na lile linaloshughulika Maendeleo (UNDP), kwa pamoja yamefanya kazi nzuri ya kuzisadia nchi kadhaa zilizo katika ukanda wa bahari ya Hindi kuboresha na kuzifanyia marekebisho sheria zake ili ziweze kubebe  jukumu hilo la kuwahukumu wahalifu wa kisomali, kwa kuzingatia sheria za kimataifa  kuhusu haki za binadamu.

“ ili juhudi hizo ziwe endelevu nchi hizi na nyingine zinatakiwa kupewa msaada wa kutosha  wa hali na mali na nchi yangu ( Uingereza ) iko tayari kusaidia wale wote waliotia sahihi  mfumo wa kanuni wa   Djibouti kuhusu sheria za kuwahukumu maharamia”.

Baadhi ya nchi hizo zipatato 10 ni pamoja na Kenya, Seychelles, Tanzania, Mauritius na Somali yenyewe. Ingawa Tanzania  imerekebisha baadhi ya sheria zake, bado haijaanza rasmi utekelezaji wa jukumu hilo kama ilivyo kwa    Kenya na Seychelles.

Karibu kila mjumbe aliyezungumza katika  mkutano huo, akiwamo mwakilishi kutoka Tanzania,alitilia mkazo wa kusaidiwa kwa nchi hizo na nyingine zitakazojitokeza kwa kile walichosema athari zitokanazo na uharamia huo  ni tishio kwa jumuia yote ya kimataifa.

Aidha baadhi ya wazungumzaji, walibainisha kwamba  ni vema pia jumuia ya kimataifa, ikajielekeza katika kutafutia ufumbuzi vyanzo au sababu zinazowafanya baadhi ya wananchi wa Somalia kujihusisha na utekaji wa meli na ujangili wa kutumia silaha bahari.

Wanavitaja vyanzo hiyo kuwa ni hali ngumu na duni kiuchumi na kimaendeleo inayowakabilia wananchi wa Somalia, kutokuwapo kwa  dola yenye mamlaka na nguvu na kutokuwapo kwa hali ya amani, usalama na utulivu.

Awali kabla ya katibu  Mkuu, Ban Ki Moon kuwasilisha ripoti yake, wajumbe wa  Baraza la Usalama walisimama kwa dakika moja kuwakumbuka wahanga wa mlipuko wa  bomu  uliotokea katika hoteli ya Muna huku Somalia na kuua watu kadhaa wakiwamo wabunge.

Akizungumzia tukio hilo, Katibu Mkuu amesema waliotekeleza uhalifu huo katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani,  siyo tu kwamba wamewaua raia wasio na hatia, lakini pia wamewakosea na kuwadharirisha waislam na watu wote wenye kupenda amani. Akasema  Umoja wa Mataifa unalaani vikali tukio hilo kwa nvugu zake zote.

Akiyataja mapendekezo yake saba ambayo anasema yakitekelezwa yanaweza kusukuma mbele  utekelezaji wa kisheria dhidi ya maharamia  na majangili ya  kisomali.  Ban Ki  Moon anaeleza kuwa katika kipindi cha miezi saba iliyopita kumekuwa na matukio  136 yanayohusishwa na vitendo vya kiharamia, huku meli zipatazo 30 zilitekwa nyara wakati meli 17 zikiwa na wafanyakazi 450 zilikuwa zimeshikiliwa na maharamia hao  wakitaka wapewe mamilioni ya fedha.

Katibu  Mkuu alizishukuru jitihada za kimataifa za kupambana na uharamia katika pwani ya Somalia, huku akisisitiza kwamba ingawa  matukio ya kiharamia  yanaelekea kama kupungua, lakini jumuia ya kimataifa inatakiwa kuongeza juhudi za kupambana na wahalifu hao.

Mapendekezo saba ambayo  Ban ki Moon aliyawasilisha mbele ya baraza Kuu ni : baadhi ni  kuundwa kwa mahakama ya Somalia, lakini itakayokuwa ikiendesha shughuli zake katika nchi ya tatu itakayokubali kuwa mwenyeji wa  mahakama hiyo.  kuwapo kwa chemba maalum katika mfumo wa sheria za nchi moja au nchi kadhaa za ukanda wa  pwani ya Somalia na pembe ya afrika kwa kushirikiana au kutoshirikiana na  Umoja wa mataifa na   , kuundwa kwa mahakama ya kikanda kwa kuzingatia makubaliano ya nchi kadhaa  huku kukiwa na ushiriki wa Umoja wa mataifa.

Mapendekezo mengine ni, kuundwa kwa mahakama ya  Kimataifa kwa kuzingatia makubaliano kati ya nchi itakayojitolea kuwa mwenyeji wa mahakama hiyo kwa kushirikiana na Umoja wa mataifa, na kuwapo kwa mahakama ya kimataifa itakayoundwa na Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa  kwa kuzingatia ibara ya VII  ya katiba ya   Umoja wa Mataifa.

Pamoja na mapendekezo hayo, ripoti hiyo pia inajadili faida na hasara zitakazotokana na utekelezaji wa mapendekezo hayo ambayo karibu nchi zote ziliyaunga mkono.